Ukarimu wa Mawakibu Husseiniyya za Karbala unatafsiriwa na urefu wa mstari wa chakula katika mkoa wa Karbala…

Maoni katika picha
Mawakibu Husseiniyya za Karbala zimeonyesha ukarimu wao kwa kuweka mistari mirefu ya chakula ndani ya mwezi wa Ramadhani kwa ajili ya mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), wahudumu wa Mawakibu wanatoa futari kwa mazuwaru katika njia zote zinazo elekea kwenye haram mbili tukufu, na mistari hiyo huwa mirefu zaidi katika usiku wa Ijumaa na siku za Lailatul Qadri, na utawaona wanashindana katika kutoa huduma bora zaidi.

Hiyo ndio kawaida ya mawakibu kila Ramadhani inapo ingia, wanafanyia kazi kauli ya Mtume (s.a.w.w) isemayo: (Atakaye mfuturisha aliye funga atalipwa sawa sawa na mfungaji bila kupunguziwa chochete), wanatumia uwezo wao wote katika kufanya jambo hili kwa ajili ya kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kupitia mmoja wa milango ya rehma, nao ni mlango wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Chakula kinacho pikwa katika mwezi wa Ramadhani hugharamiwa na kuandaliwa na wajumbe wa Mawakibu na vikundi vya Husseiniyya vya Karbala, pamoja na Mawakibu zinazo kuja kutoka nje ya mkoa, futari huandaliwa mapema sana, bila kujali joto kali lililopo pamoja na kua wamefunga, kama walivyo kua wakishindana katika kuwahudumia mazuwaru wa siku ya Ashura na Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) pamoja na minasaba mingine, hivyo hivyo leo wanashindana kuwahudumia wafungaji, mkeka wa chakula umepambwa na aina mbalimbali za vyakula vizuri pamoja na juisi na vinginevyo.

Sambamba na kuandaa chakula cha familia za mafakiri na masikini na kuwapa moja kwa moja au kwa kuwatumia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: