Kwa picha: Kundi la waumini wakiswali swala ya Idi katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)…

Maoni katika picha
Ilipo chomoza asubuhi ya kwanza katika mwezi mtukufu wa Shawwal, katika mazingira bora ya kiroho yaliyo jaa mapenzi ya Mwenyezi Mungu mtukufu, ndani ya kukumbi wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) imeswaliwa swala ya Idil-Fitri, wamejitokeza waumini wengi sana kutekeleza ibada hii na kuhitimisha funga zao zilizo ambatana na ibada mbalimbali ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Kutokana na wingi wa mazuwaru wanaokuja kutoka ndani na nje ya mkoa wa Karbala, swala ya Idi imeswaliwa zaidi ya mara moja kutokana na ufinyu wa uwanja wa haram tukufu na kwa namna isiyo weza kuzuia harakati za mazuwaru, katika swala hizo; waumini wamejikurubisha kwa Mwenyezi Mungu na kuliombea taifa la Iraq amani na usalama, na Mwenyezi Mungu awarehemu mashahidi wa Iraq pamoja na kuwaponya haraka majeruhi.

Uwanja wa eneo la katikati ya haram mbili tukufu umeshuhudia mafuriko makubwa ya watu walio jitokeza kuswali swala ya Idil-Fitri.

Watumishi wa Ataba tukufu hawakubaki nyuma katika kutoa huduma bora zaidi na kuhakikisha watu hao wanatekeleza ibada zao kwa amani na utulivu.

Tunapenda kufahamisha kua swala ya Idi ni miongoni mwa alama za uislamu, na imefungamana na ibada mbili kubwa, ambazo ni ibada ya funga na ibada ya hijja, ibada hizo huhitimishwa moja kwa moja na sikukuu za waislamu, swala ya Idi ni wajibu katika zama ambazo yupo Imamu Maasum (a.s) pamoja na kukamilika masharti, na ni sunna katika zama za ghaiba kuiswali kwa jamaa au mtu mmoja, na wala haizingatiwi idadi au umbali wa jamaa mbili, na mengineyo miongoni mwa masharti ya swala ya Ijumaa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: