Kwa mujibu wa maelezo ya Ustadh Maahir Khalidi Almiyahi ambaye ni kiongozi wa harakati za vyuo katika Atabatu Abbasiyya tukufu: “Mashindano haya yanafanyika kwa ajili ya kusaidia miradi ya kifikra na kuchochea vipawa vya kielimu, ili kuwasukuma wanafunzi kufanya tafiti za kielimu, na kuanzisha miradi yenye tija inayo weza kutekelezeka, mashindano yanalenga mambo yafuatayo:
- 1- Kuangazia mafanikio ya kiubunifu ya wanafunzi wa udaktari na uhandisi.
- 2- Kushajihisha wanafunzi na kuwajengea moyo wa kushindana baina yao na kuwasilisha mawazo yao.
- 3- Yanasaidia kugundua vipaji vya wanafunzi na kushajihisha maendeleo yao kielimu.
- 4- Kutafsiri matokeo ya tafiti za kielimu na kua tafiti za kivitendo pamoja na uwezekano wa kuzifanyia kazi.
- 5- Kuhamasisha wanafunzi kufuata nyayo za watu wa zamani za ubunifu chini ya usimamizi wa Atabatu Abbasiyya.
- 6- Kushajihisha ubunifu wa kielimu kwa wanafunzi na kusaidia tafiti za kielimu na kuzifanya kua miradi muhimu ya kumaliza masomo itakayo changia katika kujenga jamii”.
Akaongeza kusema kua: “Hakika maandalizi ya mashindano haya yameanza kitambo, tumesha fanya mikutano mingi na vyuo vikuu pamoja na kamati ya tafiti za kimaendeleo katika wizara ya elimu ya juu na utafiti wa kielimu, vikao hivyo vilituwezesha kuunda kamati ya wataalamu watakao pima na kushindanisha tafiti zitakazo shiriki katika mashindano na kutoa zawadi kwa washindi, kamati hiyo itatangazwa siku ya ufunguzi (27 Juni 2018m) na itaendelea kwa siku mbili, katika ukumbi wa jengo ya Ameed lililo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu".
akabainisha kua: “Hakika miradi itakayo shiriki katika mashindano ni ya vitendo na sio ya kwenye karatasi, zimeandaliwa zawadi za aina tatu kwa washindi watatu wa mwanzo, kama ifuatavyo:
Mshindi wa kwanza: atapata (1,500,000) milioni moja na laki tano dinari za Iraq pamoja na midani ya dhahabu.
Mshindi wa pili: atapata (1,000,000) milioni moja dinari za Iraq pamoja na midani ya fedha.
Mshini wa tatu: atapata (500,000) laki tano dinari za Iraq pamoja na midani ya burunzi.
Vile vile washiriki wote wa mashindano haya watapewa vyeti vya ushiriki.