Ndani ya siku thelathini za mwezi mtukufu wa Ramadhani, uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu umekua ukijaa mazuwaru kutoka ndani na nje ya mji mtukufu wa Karbala, uwanja huo ulibadilika na kuwa sawa na mahala pa mkutano wa kiimani ulio kua unaanza baada ya swala ya Maghribaini kwa kusoma dua ya Iftitaahi pamoja na dua zingine na ibada mbalimbali usiku mzima na kuhitimishwa kwa swala ya Alfajiri, yote hayo yalikua yanafanyika katika mazingira tulivu ya kuroho na kiusalama.
Unapo pita katika uwanja huo muda wote utawaona watu wameinua mikono wakimuomba Mwenyezi Mungu huku macho yao yakibubujika machozi, na utasikia maneno yanayo choma roho, pia utashuhudia namna watu wanavyo kusanya familia zao chini ya malalo ya bwana wa mashahidi Abu Abdillahi Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) na kufanya ibada za usiku ndani ya mwezi wa Ramadhani kwa pamoja, wakubwa, watoto, vijana, wazee, wanaume kwa wanawake, na kuomba baraka za mwezi huu mtukufu ziwafikie watu wote pamoja na wale walio shindwa kufika Karbala na kufanya ibada za usiku jirani na malalo mawili matukufu.
Kwa upande wetu Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia vitengo vyetu, tumefanya kila tuwezalo kumpatia zaairu mahitaji ya lazima anayo yataka katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani, tumewapa chakula, maji pamoja na kuandaa maeneo ya kufanyia ibada na kuweka vitabu vingi vya dua na misahafu, pia tulikua tukitoa mihadhara ya dini iliyojaa mafunzo mbalimbali sambamba na kuelezea utukufu wa siku za Lailatul Qadri na kujeruhiwa kwa kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s) pamoja na kifo chake, sambamba na kuimarisha ulinzi na kuweka mpangilio mzuri wa kuingia na kutoka mazuwaru kwa urahisi pamoja na kufurika kwao katika mji wa Karbala ndani ya siku hizi tukufu.