Picha iliyo wekwa katika habari hii, inayo muonyesha mfanyakazi wa kituo cha Alkafeel cha uzalichaji na matangazo ya moja kwa moja akiwa ameshika kikuza herufi mkononi mwake, imetusukuma –sisi wafanyakazi wa mtandao wa kimataifa Alkafeel- kuandika swala hili, kwani linamafundisho mengi hasa kwa vijana wa sasa, kutokana na maendeleo ya dunia ya karne hii –ya ishirini na moja- usomaji wa Qur’an umepungua sana katika jamii, picha hii ya (mtu mwenye umri mkubwa ameshika kikuza herufi ili aweze kusoma aya za Qur’an tukufu) inaweza kutosha na usihitaji dalili nyingine ya namna mtu huyu alivyo shikamana na kitabu kitukufu cha Mwenyezi Mungu, tukisoma hadithi ya kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s) tunakuta anasema: (Shikamaneni na kitabu cha Mwenyezi Mungu hakika ni kamba madhubuti, na nuru ya bayana, na ponyo yenye manufaa, na maji yarutubishayo, na kinga imara, na muokozi kwa mwenye kushikamana nayo, haina upungufu ili ikamilishwe wala haikosei ilaumiwe) tunaona wazi kushikamana kwa mtu huyu na kitabu hiki kitukufu.
Tukiangalia katika historia ya kiislamu, tutaona kua Qur’an inaheshima kubwa sana kwa waislamu isiyo patikana katika kitabu kingine chochote, tangu kuteremshwa kwake waliipokea kwa heshima na unyenyekevu, na wamekua wakiisoma mchana na usiku, wamehifadhi aya zake na kuwahifadhisha watoto wao, na wanazingatia maana zake na kufanyia kazi maelekezo yake.
Jambo hili ni la kawaida sana, ni kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu, kimekusanya kila aina ya uzuri, nacho kimewapa wakazi wa uwarabuni utukufu mkubwa na kuwafanya waheshimike.
Kinacho furahisha zaidi ni muamko uliopo sasa wa kurudisha roho ya kushikamana na Qur’an, hasa baada ya mabadiliko yaliyo tokea Iraq mwaka (2003), Ataba tukufu zimekua vyanzo vya harakati za kifikra na kimazingira, na zinasambaza ujumbe wa Karbala wa kibinadamu dunia nzima, miongoni mwa vipawa mbele vyao ni kufungua Maahadi na vituo vya Qur’an, na wamefanya miradi mingi ya Qur’an pamoja na mashindano ya Qur’an mara nyingi pia, mashindano ya Qur’an ya vikundi yanayo simamiwa na kituo cha miradi ya Qur’an cha Atabatu Abbasiyya tukufu, na semina za Qur’an za kiangazi kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari, na mradi wa mahafidhu elfu moja na mingineyo mingi, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu italeta muamko mzuru wa Qur’an katika taifa hili.