Msafara wa Saaqi watangaza ratiba mpya ya ziara ya malalo matukufu nchini Iran…

Idara ya kunufaika na mitambo ya Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia msafara wa Saaqi imetangaza ratiba ya safari ya Iran (kwa usafiri wa nchi kavu) ya kwenda kumzuri Imamu Ridhwa na Fatuma Maasumah (a.s) kwa muda wa siku kumi na nne (siku saba Mashhadi na siku nne Qum tukufu) ratiba hiyo inahusisha (Viza, usafiri wa basi za kisasa zenye viyoyozi kutoka Iraq hadi Iran, kukaa katika hoteli za kisasa, matembezi ya kitalii na kidini kila siku, laini ya simu kwa kila familia na milo mitatu kila siku).

Ratiba ya safari ipo kama ifuatavyo:

Siku ya kwanza: Kukusanyika katika barabara ya Maitham Tammaar- na kuondoka kuelekea katika mji wa Qum kwa mabasi ya kisasa moja kwa moja.

Siku ya pili: Kuwasili katika mji wa Qum na kukaa katika hoteli za kisasa kwa muda wa siku mbili, tutamzuru Fatuma Maasumah (a.s) na kurudi katika hoteli.

Siku ya tatu: Tutaenda katika kitongoji cha Niyaasir na kufanya matembezi ya kitalii.

Siku ya nne: Kwenda katika mji mtukufu wa Mashadi na kumzuru Imamu Ridhwa (a.s) katika kitongoji cha Nishabuur kisha tutakaa katika mji huo (Mashhadi tukufu) kwenye hoteli za kisasa kwa muda wa siku saba.

Siku ya tano: Kuzuru malalo ya Imamu Ali bun Mussa Ridhwa (a.s).

Siku ya sita: Kutembelea malalo ya maswahaba wa Imamu Ridhwa (a.s) katika (Khawajihi Rib’u + Khawajihi Muraad + Khawajihi Abuu Swilat).

Siku ya saba: Kuzuru malalo ya ndugu wa Imamu Ridhwa (a.s) Yaasir na Naaswir (a.s) kisha tutafanya ziara ya kitalii katika mji wa Shandizi na Qartwaba, halafu tutaenda katika kitongoji cha kitalii cha Kuhusanki na tutarudi kula chakula cha mchana katika mji wa Shandizi.

Siku ya nane: Mapumziko – siku ya kutembea madukani kila mtu kwa nafasi yake.

Siku ya tisa: Kutembelea malalo ya Sayyid Yahya bun Zaidi Shahidi (a.s) katika kitongoji cha Miyami.

Siku ya kumi: Matembezi ya kitalii katika mbuga ya wanyama na bustani za kupumzika pamoja na viwanja vya michezo.

Siku ya kumi na moja: Kwenda katika mji wa Tehran kuzuru malalo ya Sayyid Abdul-Adhim Hassan na Sayyid Twahir bun Imamu Zainul-Aabidina (a.s) na Sayyid Hamza bun Imamu Mussa Alkadhim (a.s), kisha tutaenda katika mji wa Qum na tutakaa katika hoteli za kisasa kwa muta wa siku mbili.

Siku ya kumi na mbili: Kutembelea mazaru tukufu za Qum miongoni mwa mazaru hizo ni (Msikiti wa Jamkarani, kaburi la nyota arubaini nao ni Ma-alawiyya 14 kutoka katika familia ya Imamu Muhammad Aljawaad (a.s), malalo ya Sayyid Mussa Mubarka’i bun Imamu Muhammad Aljawaad (a.s), malalo ya Sayyid Zaidi mjukuu wa Imamu Zainul-Aabidina (a.s) na Maqaamu ya Hidhri (a.s).

Siku ya kumi na tatu: Kujiandaa na kurudi katika mji wetu kibenzi wa Karbala, na safari itaanza baada ya Swala ya Adhuhuri.

Siku ya kumi na nne: Kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, tunatarajia kuwasiri katika mji mtukufu wa Karbala tukiwa salama.

Gharama za safari zipo kama zifuatazo:

Mtu mwenye umri wa mika (12 na zaidi) dola 300.

Mtoto mwenye umri wa miaka (2 hadi 11) dola 240.

Mtoto mdodo mwenye umri usio zidi (miaka 2) dola 75.

Kwa anaye taka kupewa chimba cha pili ni dola 50.

Kwa ajili ya kuoda nafasi ya kusafiri au kupata maelezo zaidi wasiliana na ofisi za matawi yafuatayo:

Tawi la kwanza: Mlango wa Baghdadi – Hoteli ya Aljazira ya zamani.

Tawi ya pili: Mlango wa Kibla wa Abulfadhil Abbasi (a.s), au piga simu namba zifuatazo: 07801952463 / 07602326779 / 07602327074.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: