Miongoni mwa sera zake za kushirikiana na Ataba zingine pamoja na mazaru tukufu hasa katika mambo yanayo husu utamaduni na elimu, Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia ujumbe wake rasmi imeshiriki katika hafla ya ufunguzi wa kongamano la balozi wa kitamaduni, iliyo anza jioni ya Juma Tano tarehe kumi na tano Sawwal (1439h) sawa na tarehe ishirini mwezi wa sita mwaka (2018m) linalo simamiwa na uongozi mkuu wa Masjid Kufa na mazaru zilizo chini yake, chini ya kauli mbiu isemayo: (Muslim bun Aqiil (a.s) avijuza vizazi namna ya kufikia malengo) na kuelezea mji wa Kufa ambao ulikua ni makao makuu ya uislamu, ulivyo kua zamani na sasa na kuenzi ujio wa Muslim bun Aqiil (a.s) katika mji huo akiwa ametumwa na Imamu Hussein (a.s) ambapo aliwasili Kufa tarehe tano Shawwal.
Hafla ya ufunguzi wa kongangamano imefanyika katika Muswala (ukumbi) wa balozi Muslim bun Aqiil (a.s) ndani ya msikiti mtukufu na kuhudhuriwa na viongozi wengi wa kidini na kisekula kutoka ndani na nje ya Iraq, wakiwemo wawakilishi maalumu kutoka katika Ataba na mazaru tukufu za Iraq na katika ulimwengu wa kiislamu, pamoja na wawakilishi wa serikali ya Najafu na wageni waalikwa wengine pamoja na mazuwaru watukufu.
Katibu wa msikiti wa Kufa Sayyid Muhammad Majidi Mussawi katika ujumbe alio toa, alianza kwa kukaribusha wahudhuriaji, akasisitiza kua siku ya tano katika mwezi wa Shawwal ni siku muhimu katika historia ya mji wa Kufa na huitwa siku ya Kufa, jambo hili pia linazingatiwa na bunge la mji wa Najafu na kuifanya kua rasmi, miongoni mwa maadhimisho ya siku hiyo, hukusanyika watafiti na washairi pamoja na wasanii wanao fuata mwongozo wa kitabu cha Mwenyezi Mungu na turathi za Ahlulbait (a.s) na kuelezea historia ya mji wa Kufa na harakati ya Imamu Mahdi (a.f), mji wa Kufa ni alima ya Mwenyezi Mungu na fuvu la waarabu pia ni lulu ya imani.
Rais wa uongozi wa wakfu Shia Sayyid Alaa Mussawi katika ujumbe wake amewataka watafiti na wanahistoria kuzijibu kalamu za wapotoshaji zinazo andika kua mji wa Kufa ni mji wa vitimbi, wanasahau namna mji huo ulivyo pambana na matwaghuti pamoja na maadui wa Ahlulbait (a.s) na kushikamana kwao na uislamu halisi wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), akausifu mji wa Kufa kua ni mji wa wastaarabu katika historia ya kiislamu na katika historia ya Iraq, ni mji ambao ulibadilisha muelekeo na kuifanya Iraq kua shina la waarabu na msingi wa tamaduni za kiislamu.
Pembezoni mwa hafla ya ufunguzi wa kongamano baadhi ya watu wa Kufa wamepewa zawadi, na umefanyika ufunguzi wa maonyesho ya hati za kiarabu na picha pamoja na vitabu vinavyo elezea historia ya mji huo mtukufu.