Kwa kuhudhuria kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Husseiniyya tukufu: Kamati ya maandalizi ya kongamano la Rabiu Shahada yatoa zawadi kwa wajumbe wake...

Maoni katika picha
Ndani wa ukumbi mtukufu wa haram ya Imamu Hussein (a.s), na kwa kuhudhuria kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Husseiniyya Mheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai na katibu wake mkuu Sayyid Jafari Mussawi, wajumbe wa kamati wa kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada ya kumi na nne iliyo fanyika chini ya kauli mbiu isemaye: (Tumepigana kwa utukufu wa Hussein (a.s) na tumeshinda kwa utukufu wa fatwa) lililo fanyika katika mwezi wa Shabani, imetoa zawadi kwa wajumbe wake, kutoka na kazi nzuri walizo fanya, zilizo pelekea kufanikiwa kongamano hilo la kitamaduni chini ya mazingira mazuri yaliyo onyesha utamaduni wa Husseiniyya walio nao watu wa mji wa Imamu Hussein (a.s).

Shekh Karbalai katika hafla hiyo ametoa pongezi kubwa kwa wajumbe wa kamati ya maandalizi kwa utendaji wao mzuri ulio onekana wazi katika utekelezaji wa vipengele za kongamano hilo, na akahimiza waendelee kudumisha mafanikio hayo katika makongamano yajayo, akasema kua, kumalizika kwa kongamano la kumi na nne uwe mwanzo wa maandalizi ya kongamano la kumi na tano.

Mjumbe wa kamati ya maandalizi na raisi wa kitengo cha habari katika kamati hiyo, Sayyid Aqiil Abdul-Hussein Yasiri ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Hakika swala la kupewa zawadi kamati ya maadalizi ya kongamano la Rabiu shahada sio geni, inatokana na kazi nzuri walizo fanya iliyo pelekea kufanikiwa kwa kongamano hilo, tena kwa mujibu wa ushahidi kutoka kwa kila aliye hudhuria na kushiriki katika kongamano, ukizingatia kua lilikua la aina yake, kwani ni kongamano la kwanza kufanywa baada ya kukomboa ardhi yote ya Iraq kutoka mikononi mwa magaidi wa Daesh, kutokana na ushindi wa wairaq dhidi ya magaidi, jambo hilo tumeliashiria katika kauli mbiu ya kongamano na tukaliingiza katika vipengele vya ratiba ya kongamano”.

Kumbuka kua kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada linalo andaliwa na kusimamiwa na Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya kila mwaka kwa ajili ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mjukuu wa Mtume (s.a.w.w) Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi na Imamu Sajjaad Zainul-Aabidina (a.s) ni moja ya makongamano makubwa yanayo fanywa kwa ushirikiano wa Ataba mbili tukufu kila mwaka, huzingatiwa kuwa kitu muhimu katika harakati za kitamaduni ndani ya jamii na lina faida kubwa sana kidini, pia linasaidia kubainisha muhanga wa Imamu Hussein kwa kuuelezea kwa namna maalumu, kongamano la mwaka huu limehudhuriwa na wawakilishi kutoka nchi 33 duniani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: