Chini ya kauli mbiu isemayo: (Tunaandika historia yetu kwa mikono yetu.. ili isipotoshwe na wengine) na kwa ajili ya kuenzi kujitolea kwa majemedari wa Hashdi Sha’abi na wanajeshi wa serikali, Atabatu Husseiniyya tukufu kupitia kitengo cha harakati na kwa kushirikiana na kituo cha kimataifa cha utamaduni na usanii nchini Iraq wanafanya kongamano la (Waitikiao), na kuhudhuriwa rasmi na ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu, asubuhi ya Akhamisi ya tarehe (6 Shawwal 1439h) sawa na (21 Juni 2018m) na litaendelea kwa muda wa siku sita, katika kongamano hili la (Waitikiao) kutakua na mashindano ya sanaa na ya kiuandishi, kuna vikundi zaidi ya (350) vinavyo shiriki kutoka nchi (12) za kiarabu na kiajemi bila kuisahai Iraq.
Kongamano hili linafanyika kwa ajili ya kuangalia na kuenzi mambo yaliyo fanywa na majemedari wetu katika vita ya kukomboa miji iliyo kua imetekwa na magaidi, namna wanajeshi wa serikali na Hashdi Sha’abi walivyo heshimu haki za binadamu.
Kwa mujibu wa maelezo ya Ustadh Ali Kaadhim Sultani, ambaye ni rais wa kitengo cha harakati cha Atabatu Husseiniyya tukufu: “Kongamano hili linalenga kuenzi na kuthibitisha kujitolea kukubwa kuliko fanywa na majemedari wa Hashdi Sha’abi na wanajeshi wa serikali, na mashindano yanayo simamiwa na Atabatu Hueesiniyya kwa kushirikiana na kituo cha kimataifa cha utamaduni na sanaa ambayo ni miongoni mwa ratiba za kongamano, yamepata mwitikio mkubwa kutoka ndani na nje ya Iraq, hakika Atabatu Husseiniyya tukufu kutokana na maelekezo ya Marjaa dini mkuu, imelipa umuhimu mkubwa sana swala la kujitolea kwa majemedari walio itikia wito wa Marjaiyya wa kuilinda Iraq na maeneo matukufu, mambo yanayo zingatiwa katika konganano ni: Fani za kiuandishi, kama vile ripoti bora ya gazeti, na ripoti bora ya kwenye tv (luninga) na fani ya uchoraji wa picha pamoja na mashindano ya mashairi ya Umudi na Sha’abi”.
Kiongozi wa kamati ya habari ya kongamano hilo, Ustadh Hussein Ni’imah amesema kua: “Kongamano hili litadumu siku sita, kutakua na mashindano ya fani ya uandishi, lugha na sanaa, vikundi vinavyo shiriki katika kongamano ni zaidi ya (350) kutoka katika nchi (12) za kiarabu na kiajemi, upekee wa kongamano la mwaka huu ni kwamba watalamu wa lugha, waandishi na watu wa sanaa woto wameungana katika kuonyesha ushindi wa wananchi wa Iraq dhidi ya magaidi wa Daesh”.
Akasema kua: “Kamati kuu ya kongamano hili imeteua kamati ya majaji walio bobea katika sekta zinazo shiriki katika mashindano, ambazo ni sekta ya lugha, ambayo itakua na visa vifupi, maigizo na mashairi, sekta ya pili ni uandishi bora, inayo husisha ripoti za kwenye tv (luninga) na za kwenye magazeti pamaja na nakala za picha, na sekta ya tatu inahusisha uchoraji, ubunifu, hati na mapambo, pia kongamano linahusisha maonyesho yanayo fanyika katika eneo lililo pauliwa katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, pia katika maonyesho hayo kuna baadhi ya siraha zilizo tekwa na wapiganaji wa kikosi cha Ali Akbaru na kikosi cha Abbasi cha wapiganaji katika vita dhidi ya magaidi wa Daesh”.