Maandalizi ya awamu ya tatu ya kongamano la fatwa tukufu ya kujilinda yanaendelea na kamati ya maandalizi yasema yatakua na vipengele ambavyo havikuwepo awali…

Maoni katika picha
Kamati ya maandalizi ya kongamao la fatwa tukufu ya kujilinda linalo andaliwa na kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu kwa ajili ya kukumbuka fatwa ya kihistoria iliyo tolewa na Marja dini mkuu ya kuilinda Iraq na maeneo matukufu, imesema kua awamu ya tatu na kongamano hilo itakua ya aina yake, kwani litakua na vipengele vinavyo husu fatwa hiyo ilivyo, na mwitikio iliyo pata kwa raia wa Iraq, na ushindi wao dhidi ya magaidi wa Daesh pamoja na namna walivyo komboa maeneo yote yaliyo kua yametekwa na magaidi.

Mjumbe wa kamati ya maandalizi na makamo rais wa kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu Ustadh Ahmadi Swaadiq akaongeza kusema kua: “Hakika kongamano litakalo fanyika chini ya kauli mbiu isemayo: (Ushindi umetokana na nyie ni wenu na nyie ndio washindi) mwaka huu lina uzuri wake, kwani linafanyika wakati ambao ardhi yote ya Iraq imesha kombolewa, ushindi huu umepatikana kwa utukufu wa fatwa iliyo tolewa na Marjaa dini mkuu Sayyid Ali Sistani na mwitikio mkubwa wa raia wa Iraq, jambo lililo tusukuma kuandaa ratiba yenye vipengele maalumu vitakavyo ongeza uzuri wa kangamano hilo”.

Akabainisha kua: “Kongamano litafanyika tarehe (28 na 29 Juni) litakua sawa na sehemu ya kuwakumbuka na kuwatambua mashahidi na majeruhi walio jitolea uhai wao kwa ajili ya ardhi ya taifa hili kipenzi, kutakua na vipengele vingi, miongoni mwa vipengele hivyo ni:

Kwanza: Yatatangazwa matokeo ya mashindano yaliyo tangazwa siku za nyuma, ambayo ni mashindano ya filamu, Makala, utafiti na picha.

Pili: Kutangaza na kuzindua kitabu cha fatwa tukufu ya kujilinda kitakacho tolewa na kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu.

Tatu: Uzinduzi wa maonyesho ya picha na machapisho yatakayo kua katika eneo la katikati ya haram mbili tukufu.

Nne: Kutakua na kisomo cha Qur’an na cha mashairi.

Tano: Kufanyika kongamano maalumu kuhusu jinai ya zama (Mauwaji ya Sipaika) litahusisha vitu vingi ikiwa ni pamoja na: Kuwasilishwa kwa jumbe mbalimbali, kuonyesha filamu na kutoa zawadi kwa familia za mashahidi hao na wale walio salimika katika mauaji hayo.

Sita: Kufanya kongamano maalumu la kitafiti, chini ya kauli mbiu isemayo: (Marjaa dini mkuu ni ngao ya umma wa kiislamu), na zitawasilishwa tafiti zilizo faulu katika shindalo la tafiti kwa mujibu wa kamati ya maandalizi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: