Makumbusho ya Alkafeel ya vifaa na nakala kale yashiriki katika kongamano la (Waitikiao)…

Maoni katika picha
Miongoni mwa ushiriki wake katika kongamano la (Waitikiao) linalo simamiwa na Atabatu Husseiniyya tukufu katika maonyesho yanayo fanyika ndani ya uwanja wa eneo la katikati ya haram mbili tukufu, makumbusho ya Alkafeel imeonyesha orodha kadhaa ya vifaa vya wapiganaji wa Hashdi Sha’abi walio shiriki katika vita ya kukombo miji ya Iraq kutoka kwa magaidi wa Daesh, vifaa walivyo viteka kutoka kwa magaidi hao na wakaipa makumbusho hii tukufu.

Makamo rais wa kitengo cha makumbusho ya Alkafeel Ustadh Sajjaad Hassan Ali ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Hakika ushiriki wa makumbusho ya Alkafeel katika maonyesho haya ni fursa ya kuonyesha vifaa vya kivita ilivyo zawadiwa na wapiganaji wa Hashdi Sha’abi, miongoni mwa vifaa hivyo ni bunduki na mapanga ya magaidi wa Daesh, ambao walitumia siraha hizo katika kufanya mauwaji ya kinyama mno kwa watu wasio kua na hatia”.

Akaongeza kusema kua: “Kitu kikubwa kinacho onyeshwa na makumbusho yetu ni pikipiki ya Shahidi wa kikosi cha Ali Akbaru (a.s) Abu Tahsiin Swaalehiy (r.a) pamoja na idadi kubwa ya picha zinazo onyesha vifaa vilivyopo katika makumbusho”.

Akaendelea kusema kua: “Ushiriki huu ni sehemu ya kusapoti juhudi za wanajeshi wa serikali na Hashdi Sha’abi walio onyesha ushujaa wa hali ya juu dhidi ya magaidi na wakafanikiwa kukomboa ardhi ya taifa letu tukufu”.

Kumbuka kua kongamano la (Waitikiao) linalo simamiwa na Atabatu Husseiniyya tukufu lilianza Adhuhuri ya jana Alkhamisi chini ya kauli mbiu isemayo: (Tunaandika historia kwa mikono yetu.. ili isipotoshwe na wengine) likiwa na washiriki zaidi ya (350) kutoka katika nchi (12) za kiarabu na kiajemi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: