Tarehe nane Shawwal ni jeraha la Baqii ambalo alijapona na halitapona pamoja na kupita muda mrefu…

Maoni katika picha
Baqii ni jeraha ambalo halijapona na halitapona pamoja na kupita miaka mingi.. Baqii ni kielelezo cha wazi kua ni sehemu iliyo teuliwa kuwatoa watu katika giza na kuwaingiza katika nuru, ikashambuliwa na watu waovu na maibilisi wa kibinadamu wakavunja na kusambaratisha kabisa mazaru zao.

Machungu ya kuvunjwa kwa Baqii bado yapo katika nyoyo za wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s), kila mwaka huhuisha huzuni zao kwa kukumbuka jinai zilizo fanywa na kundi la Mawahabi za kuvunja makaburi ya Maimamu wa watu wa nyumba ya Mtume watakatifu (a.s), na kuvunja heshima yao na utukufu wao kwa kufanya mashambulio mara mbili.

Mara ya kwanza: Mwaka (1220h) walifanya unyama ambao hauta sahaulika, wakati wa kuanzishwa kwa dola ya Saudia ya kwanza, hapa Baqii ilivunjwa kwa mara ya kwanza mwaka wa (1220h), walipo angushwa na utawala wa Othumaniyya, waislamu wakarudia kujenga tena, wakajenda kubba na misikiti kwa ufundi na umaridadi mkubwa, sehemu hiyo ikarudisha heshima yake na watu wakawa wanakwenda kufanya ziara baada ya kuondoshwa kwa Mawahabi kwa muda fulani.

Mara ya pili: Mwaka wa (1344h) Mawahabi walirudi kuushambulia tena mji wa Madina, katika mwaka wa (1344h) baada ya kusimamisha utawala wao kwa mara ya tatu, wakavunja sehemu zote tukufu za Maimamu watakatifu (a.s) na watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w), baada ya kuzidharau na kuzikejeli fatwa zilizo wakataza kufanya hivyo, walivunja makaburi na misikiti yote iliyo kuwepo Baqii hadi ukawa sawa na uwanja wa mpira kiasi hauwezi kujua sehemu palipokua kaburi.

Waliyavunja makaburi ya Maimamu wanne watakatifu (a.s) na wakafuta athari zote za Ahlulbait (a.s), wakaiba vitu vyote vya thamani, hakuna kilicho salimika ispokua kaburi la Mtume (s.a.w.w) peke yake, waliiba mali zote zilizo kuwepo hazina.

Sambamba ya hayo walivunja pia makaburi mengine, kama vile kaburi linalo chukuliwa kua ni la bibi Fatuma Zaharaa (a.s), kaburi la Ummul Banina (a.s), Kaburi la Ibrahim mtoto wa Mtume (s.a.w.w), kaburi la Ismaiil mtoto wa Imamu Jafari Swaadiq (a.s), kaburi la Halima Saadiyya mnyonyeshaji wa Mtume (s.a.w.w), kaburi la Hamza bun Abdulmutwalib (a.s) pamoja na makaburi ya mashahidi wa vita ya Uhudi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: