Ewe umma wenye majeraha njoo Baqii, kuomboleza makaburi yasiyo kua na miili, yamevunjwa na mikono ya wajinga madhalimu, wasio jua heshima ya makaburi, wala hawajui kuwa heshima ya muumini ni kubwa mno zaidi ya heshima ya Kaaba na mazaru… mtu anayetaka kuvunja heshima ya mtu, historia yake na alama zake.. ni mtu muovu mno anaye vunja kaburi lake.. na makazi yake ya mwisho.. Mtume wa rehema (s.a.w.w) anasema: (Amani iwe juu yenu enyi nyumba za watu mlio amini, ewe Mola wasamehe watu wa Baqii Gharqad).
Mara ngapi alikua akiwatakia rehma na kuwaombea dua watu hao.. Baqii inahistoria za makarama, iliyo andikwa na watukufu wake mashahidi, nayo imebeba watukufu ambao nuru zao zimeangazia vizazi na vizazi wa waislamu, wakiwakumbuka mababu zao walio lingania dini ya Muhammadiyya (uislamu).. na athari za Utume na kizazi chake kitakatifu, watu walio amini ahadi ya Mwenyezi Mungu kwao, na hekima ya ujumbe wa mbinguni (Uislamu) usemao: (Tembeleeni makaburi hakika yanakukumbusheni mauti).
Baqii inaita na majeraha yake yanaita: nyumba za wahyi na utukufu wallahi zimevunjwa, hawakuheshimu utukufu wake, wakati imejaa nyayo za Mtume.. wallahi hawakuogopa dhimma, wamevunja heshima za aya za Qur’an.
Hakika waliifanyia ukatili –kwa mujibu wa maneno ya mbora wa mawasii- alipo kua akielezea utukufu wake.. na umuhimu wake.. na wingi wa athari zake.. uovu ulioje na dhulma, zilizo fanywa na makundi maovu, yalio tupa kitabu, wakaabudu matwaghuti na dola (pesa).. waliuza turathi zetu, wakavunja malalo yetu, wakatutenganisha.. ili tusipate shifaa na maombezi…
Tunaingia eneo la Baqii na tumuulize majeruhi Qharqad: kuhusu mashambulizi ya waovu.. watu wakufurishaji?! Atatujibu kwa unyonge: Naam wallahi, wamefanya uwovi na kuvunja… kikundi cha maluuni, na njama za kijinga, Baqii ilijengwa na watu wema, leo hii waovu wamekuja kuivunja..
Maini yalikatwa katwa jana.. leo wanakuja kuvunja vunja makaburi.. kama kwamba nipo katika nyumba ya huzuni navaa sanda: watu waovu wameizunguka Baqii, wakiwa na mapanga mikononi mwao, wanawazuia watu wema kuingia, na wanafanya hasara!!
Hadi machozi yameanza kuwaogopa matwaghuti, tujaze bustani mito ya upendo, na tunywesheleze kiu ya Baqii huwenda Sidra utawapa kivuli, leo hii inaingia misafara ya waombolezaji.