Watumishi wa Abalfadhil Abbasi (a.s) wanaita waa Baqiiaahu…

Maoni katika picha
Tangu miaka (90) iliyo pita maadui wa Ahlulbait (a.s) miongoni mwa Mawahabi walifanya jinai kubwa sana dhidi ya turathi za kiislamu na kibinadamu, walivamia moja ya sehemu muhimu sana kwa wapenzi wa watu wa nyumba ya Mtume (a.s), walivunja makaburi ya familia ya Mtume (a.s.w.w), mabwana wa viumbe na makhalifa wa haki, walio ifanya ardhi hiyo kuwa tukufu baada ya kuzikwa miili yao mahala hapo, na pakawa ni nuru inayo waongoza waislamu, kuanzia kwa mjukuu wa Mtume na bwana wa vijana wa peponi Imamu Hassan Zakiy kisha Maulana Zainul-Aabidina na Imamu Sajjaad huku pembezoni mwake akiwa kazikwa mwanaye Imamu Baaqir na Jafari Swaadiq (a.s), wakiwa wamezungukwa na makaburi ya waja wema, watu wa familia zao na maswahaba zao watu ambao wamejaa katika historia ya kiislamu.

Wafuasi wa Bani Umayya wakalibadilisha eneo hilo na kua sawa na ardhi tupu, baada ya kua waumini kutoka kila sehemu walikua wanafunga safari kwenda eneo hilo, zilikua zinasikika sauti za dua na ziara pamoja na kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu mtukufu, ilikua kimbilio la waislamu walio kuwa wakijua umuhimu wa kuwaenzi watukufu walio zikwa katika eneo hilo, watu wanaojua maana ya tauhidi na imani walio jitolea katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kuunusuru uislamu.

Kwa ajili ya kukumbuka tukio hili linalo umiza roho ya Imamu wa zama zetu Hujjat bun Hassan (a.f) pamoja na wafuasi wake, watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wamehuisha kumbukumbu ya kuvunjwa makaburi ya Maimamu wa Baqii, tukio lilito fanyika tarehe nane ya mwezi wa Shawwal mwaka wa (1344h) wakakumbuka maovu yaliyo fanywa na mawahabi, kutokana na chuki zao kwa familia ya Mtume (s.a.w.w) na kwa wafuasi wao na wapenzi wao, kikundi cha waombolezaji kimefanya matembezi kutoka katika haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi hadi katika haram ya ndugu yake Imamu Hussein (a.s), huku wakiimba kaswida za kumpa pole bibi Zaharaa (a.s) kutokana na msiba huu, na wakisema: Waa Baqi’aahu waa muswibataahu.

Baada ya hapo walifanya majlisi ya kuomboleza ndani ya haram tukufu ya Imamu Hussein kwa kushirikiana pamoja watumishi wa Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya) pamoja na mazuwaru, wakaimba kaswida zilizo onyesha ukubwa wa msiba huu, na kumpa pole bwana wa mashahidi (a.s) pamoja na Maulana Imamu wa Zama (a.f) na kuomba adhihiri haraka na kulipa kisasi kwa maadui wa nyumba ya Mtume (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: