Kwa ufadhili wa Atabatu Abbasiyya tukufu na kushirikiana na mafundi wa Atabatu Husseiniyya tukufu na ofisi ya maji ya mkoa wa Karbala, kitengo cha usimamizi wa kihandishi cha Atabatu Abbasiyya tukufu kinashiriki katika uanzishwaji wa kituo cha kusambaza maji katika nyumba na mawakibu za Husseiniyya pamoja na makundi ya watu wanao toa huduma kwa mazuwaru katika barabara ya (Yaa Hussein) iliyopo kati aya Najafu na Karbala tukufu".
Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi cha Atabatu Abbasiyya, Mhandisi Abbasi Mussa Ahmadi: “Mradi huu unaingia katika orodha ya miradi inayo fanywa na Ataba tukufu, na wasimamizi wa utekelezaji wake ni mafundi na wahandisi wa kitengo chetu, mradi huu unakusudia kupeleka maji safi ya kunywa katika barabara ya (Yaa Hussein) na maeneo ya kutolea huduma kama vile katika mawakibu za Husseiniyya, uwanja wa ndege, machinjioni pamoja na miji ya mazuwaru na kwa wakazi wa barabara hiyo pamoja na vyuo na majengo ya makazi ya Abbasi”.
Akaongeza kusema kua: “Kabla ya kuanza utekelezaji wa mradi huu, tulianza kufanya upembuzi wa mradi, kisha tukaandaa mpango kazi, baada ya kupasishwa ndio tukaanza utekelezaji wa mradi, tumeanza kwa kujenga nyumba za chini pamoja na kuziwekea vifaa vya kikemia katika eneo lenye ukubwa wa (2m1000), vilevile tumeweka mabomba na tumechimba vituo vya mabomba vyenye ubora unaokubalika kitaifa”.
Akabainisha kua: “Hakika kituo cha usambazaji wa maji kinaweza kusambaza (3m200/ kwa saa), sasa hivi kazi inaendelea na imesha fika hatua nzuri, kukamilika kwa kazi hii kutamaliza tatizo kubwa lililo kuwepa kwa wakazi wa maeneo hayo la ukosefu wa maji safi ya kunywa na hali ilikua mbaya zaidi katika siku za ziara.