Kamati ya maandalizi ya fatwa tukufu ya kujilinda itakayo anza Ijumaa ijayo chini ya kauli mbiu isemayo: (Ushindi umetokana na nyie ni wenu na nyie ndio washindi) imetangaza kukamilika kwa uchambuzi wa tafiti za kielimu zitakazo shiriki katika kipengele cha tafiti kilichopo katika ratiba ya kongamano na kinacho chukuliwa kua muhimu zaidi, wakasisitiza kua; tafiti ni nzuri na zimekusanya mtazamo wa kisekula na kihauza na zinaendana na viwango vya makongamano ya kitafiti.
Akaongeza kusema kua: “Idadi ya tafiti zilizo pokelewa zilikua (58) za kisekula na kihauza kutoka ndani na nje ya Iraq, tafiti zote zikakabidhiwa kamati ya wasomi kwa ajili ya kuzifanyia mchujo, kamati hiyo imepasisha tafiti (28) katika hizo tafiti tano za kwanza ndio zitapewa zawadi za ushindi katika shindano la tafiti”.
Kumbuka kua kongamano hili linasimamiwa na kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu kwa ajili ya kuhuisha kumbukumbu ya fatwa ya kihistoria iliyo tolewa na Marjaa dini mkuu katika mji wa Najafu, fatwa iliyo linda Iraq na maeneo matakatifu kutokana na uwadui wa magaidi wa Daesh, na ikaferisha njama zao kufuatia mwitikio wa haraka wa wananchi watukufu wa Iraq, kongamano litakua na vipengele mbalimbali na litadumu siku mbili.