Kitengo cha malezi na elimu ya juu chafanya warsha ya kuwajengea uwezo watumishi…

Maoni katika picha
Kitengo cha malezi na elimu ya juu cha Atabatu Abbasiyya tukufu chafanya warsha ya kuwajengea uwezo watumishi wake chini ya anuani isemayo: (Namna ya kushirikiana na marafiki na kuleta athari), warsha hii ni sehemu ya orodha ya semina na warsha zinazo tolewa na kitengo hicho kwa watumishi mbalimbali sawa iwe katika sekta ya kielimu au kiofisi, kwa ajili ya kuwajengea uwezo katika utendaji wao na kuwafanya waendane na maendeleo yanayo patikana katika vitengo vyao.

Warsha hii inawashiriki (40) kutoka vitengo mbalimbali na inasimamiwa na Dokta Hassan Jadhili, ametuelezea kuhusu warsha hii kua: “Warsha ya kimasomo ni sehemu ya kuwajengea uwezo watumishi, tumewafundisha namna tisa muhimu zinazo elekezwa na elimu ya nasfi katika utumishi, ikiwemo: kuonyesha heshima na namna ya kufahamu mtazamo wa watu wengine, pamoja na njia ya kutilia umuhimu jambo linalo shirikisha watu wengine na kujitenga na jambo lenye utata na linalo weza kuwagawa watu kazini, pia tumewafundisha namna ya kufikiri fikra zenye tija, pamoja na mafunzo ya njia za kutoa maoni na kupunguza baadhi ya misimamo”.

Akabainisha kua: “Washiriki wametoka katika vitengo tofauti, na wote wameonyeshwa kuguswa na mada zilizo fundishwa, na wametoa ushirikiano mkubwa kwa kueleza mifano tofauti kutoka katika vitengo vyao, tulijitahidi sana kutafuta mada zinazo endana na mazingira halisi ya walengwa ili kuwafanya wafaidike zaidi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: