Katika muendelezo wa miradi ya Qur’an inayo lenga kueneza utamaduni wa Qur’an tukufu katika nyoyo za vijana, Maahadi ya Qur’an chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu cha Atabatu Abbasiyya, inaendesha mradi wa (Semina za Qur’an za msimu wa kiangazi) katika makao makuu yake na kwenye matawi yake yaliyopo karibu mikoa yoye ya Iraq, kwa ajili ya kuhakikisha wana nufaika na kipindi cha likizo za kiangazi, na kujaribu kutengeneza kizazi cha watu wanao fuata tamaduni halisi za kiislamu zitokanazo na Qur’an tukufu na kizazi cha Mtume kitakatifu.
Mkuu wa Maahadi ya Qur’an tukufu katika Atabatu Abbasiyya Shekh Jawadi Nasrawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Semina hizi ni muendelezo wa semina zilizo fanywa na Maahadi kwa lengo la kuandaa kizazi cha vijana wanaofuata tamaduni za Qur’an na mwenendo wa Ahlulbait (a.s), hakika kutoa elimu ya Qur’an katika jamii ni jambo muhimu sana na linasaidia kupambana na maadui wa dini, nao ni miongoni mwa miradi muhimu inayo pewa nafasi kubwa na Maahadi ya Qur’an tukufu, pia Atabatu Abbasiyya inatoa kipawa mbele kikubwa katika miradi ya Qur’an kutokana na umuhimu wake wa kutakasa nafsi”.
Akaongeza kusema kua: “Mradi huu utakao dumu siku (40) unahusisha masomo mengi, likiwemo somo la kuhifadhi Qur’an tukufu, masomo ya Fiqhi na Aqida, watafundishwa pia mizizi ya dini na nguzo za uislamu kwa ujumla, sambamba na masomo ya Akhlaqi, na somo la lazima kwa wanafunzi wote ni kufundishwa swala sahihi na namna ya kutawadha, kuoga na kutayamamu”.
Tunatumia Sardabu (kumbi za chini) za Atabatu Abbasiyya kwa kufundishia washiriki wanao ishi karibu na haram tukufu, na tumewagawa wanafunzi katika makundi kwa ajili ya kupata urahisi wa kuelewa masomo, masomo huanza saa tatu asubuhi hadi saa sita Adhuhuri, kila siku wanafundishwa masomo manne ispokua Alkhamisi na Ijumaa, baada ya masomo wanafunzu hurudishwa makwao kwa mabasi ya Ataba tukufu, pia Ataba imewashonea sale.
Kumbuka kua mradi huu ni wa aina yake, unalenga kuandaa kizazi kinacho fuata mwenendo wa vizito viwili –Qur’an tukufu na kizazi cha Mtume kitakatifu- idadi ya washiriki inaendelea kuongezeka mwaka baada ya mwaka, mwaka 2011 mradi ulianza na wanafunzi (150) ulipo fika mwaka 2014 wakaongezeka hadi zaidi ya wanafunzi (6000) na katika mwaka 2016 wakawa zaidi ya wanafunzi (10,000), wakaendelea kuongezeka hadi mwaka 2017 tulikua na wanafunzi zaidi ya elfu kumi na sita.