Katika mahudhurio makubwa ya wasomi wa sekula na wa dini: Chuo kikuu cha Ameed chawa mwenyeji wa hafla ya mashindano ya kijana wa Alkafeel ya ubunifu wa kifikra kwa wahitimu wa udaktari na uhandisi wa vyuo vya Iraq…

Maoni katika picha
Ukumbi wa chuo kikuu cha Ameed asubuhi ya Juma Tano (12 Shawwal 1439h) sawa na (27 Juni 2018m) umekua mwenyeji wa hafla ya ufunguzi wa mashindano ya kijana wa Alkafeel ya ubunifu wa kifikra kwa wahitimu wa udaktari na uhandisi wa vyuo vikuu vya Iraq, linalo simamiwa na idara ya mahusiano ya vyuo chini ya kitengo cha mahusiano cha Atabatu Abbasiyya tukufu na usimamizi mahiri wa katibu mkuu Sayyid Muhammad Ashiqar, pamoja na ushiriki wa serikali ikiwakilishwa na idara ya utafiti na maendeleo ya kielimu katika wizara ya elimu ya juu na utafiti wa kielimu, pamoja na mahudhurio makubwa ya walimu wa vyuo vikuu na idadi kubwa ya wanafunzi washiriki.

Hafla imefunguliwa kwa Qur’an tukufu iliyo fuatiwa na kisomo cha surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi watukufu wa Iraq, halafu ukafuata wimbo wa taifa na wimbo wa Atabatu Abbasiyya tukufu, kisha likafuata tamko la kukaribisha wageni lililo tolewa na raisi wa chuo Dokta Jaasim Marzuqi ambaye alisema kua: “Hakika ni fahari kubwa sana ukumbi huu kua mwenyeji wa hafla hii, chuo kikuu cha Ameed ni tunda la Atabatu Abbasiyya tukufu la kimalezi na kielimu kinatoa masomo ya awali (chekechea) hadi chuo kikuu”.

Akaongeza kusema kua: “Leo tunakaribisha mradi huu wa kijana mzalendo wa Alkafeel unao husu ubunifu wa kifikra unao onyesha elimu ya wanafunzi wetu wa udaktari na uhandisi kupitia kazi zao za kuhitimu masomo, tunawakaribisha pamoja na walimu wao watukufu ndani ya chuo hiki, tunawakaribisha sana, tuna matumaini makubwa na mradi huu, tunatarajia miaka ijayo kualika mashirika kwa ajili ya kuja kuangalia namna ya kunufaika na miradi hii ambayo ni tafiti zinazo kuja na majibu ya changamoto za taifa hili, na kuleta utatuzi wa changamoto hizo na hili ni jambo linalo furahisha kwa kweli”.

Baada yake ukafuata ujumbe wa ofisi ya utafiti na maendeleo ya kielimu wa wizara ya elimu ya juu na utafiti wa kielimu ya Iraq, ulio wasilishwa na mkuu wa kitengo cha miradi ya kielimu Dokta Yusufu Khalfu Yusufu, ambaye amesema kua: “Miongoni mwa fahari na furaha kubwa ni kushuhudia mashindano ya kielimu kama haya, ambayo wahitimu wa Udaktari na Uhandisi kutoka vyuo vikuu vya Iraq katika maeneo tofauti wanachuana, na jambo zuri zaidi ni mashindano haya kuandaliwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, na kufanyika katika chuo cha Ameed, hakika ni fursa nzuri kwa wizara na wanafunzi kushuhudia tukio hili tukufu la kielimu”.

Akaendelea kusema kua: “Wizara ya elimu ya juu kupitia ofisi ya utafiti na maendeleo kitengo cha miradi ya kielimu imetoa ushirikiano katika kuandaa mashindano haya, kwa kusaidia kuunda kamati ya walimu walio bobea katika masomo ya kisekula, na wenye uwezo mkubwa wa kuchambua na kujaji tafiti za kielimu zinazo shiriki katika mashindano haya, hivyo wizara ya elimu ya juu na utafiti wa kielimu imeshiri moja kwa moja katika jambo hili”.

Akakamilisha kwa kusema: “Wizara inatumia kipimo cha kielimu katika kujaji tafiti zilizo wasilishwa katika mashindano haya, kwa kuziangalia kwa kiasi gani zinatatua changamoto zilizopo, kwa kusoma miradi iliyo andikwa na kuangalia uhalisia wake kama inaweza kutekelezwa kwa vitendo au ni ya kufikirika tu, na kuangalia faida inayo weza kupatikana iwapo miradi hiyo ikitekelezwa”.

Akafafanua kua: “Katika kujaji kazi hizi tumesha kamilisha sehemu muhimu, ambayo ni kutembelea eneo la mradi na kumuhoji mwanafunzi ili kupima uwelewa wake kuhusu mradi alio andika na namna ya utekelezwaji wa mradi huo na una mazuri gani na mapungufu gani”.

Akamaliza kwa kusema: “Natarajia Atabatu Abbasiyya tukufu itajalia mashindano haya kua mwanzo wa kuelekea katika mashindano makubwa yakakayo husisha wanafunzi wengi zaidi wa elimu za juu, akarudia kutoa shukrani kubwa kwa Atabatu Abbasiyya na kwa chuo kikuu cha Ameed kwa kuandaa mashindano haya”.

Mwishoni mwa hafla hiyo ukatangazwa ufunguzi wa maonyesho maalumu ya tafiti za kitabibu na kihandisi zilizo fanywa na wanafunzi wa vyuo vya Iraq, wahudhuriaji walitembelea meza za maonyesho hayo, na kila mtafiti alielezea utafiti wake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: