Kamati ya maandalizi ya mkutano wa waandishi wa habari wanawake wa mwaka wa tatu yakamilisha maandalizi ya mwisho ya mkutano huo…

Maoni katika picha
Kamati ya maandalizi ya jarida ya Riyadhi Zaharaa yakamilisha maandalizi ya mwisho ya mkutano wa waandishi wa habari wanawake wa mwaka wa tatu unao tarajiwa kufanywa siku ya Ijumaa (14 Shawwal 1439h) sawa na (29 Juni 2018m).

Mkuu wa ofisi ya wanawake na rais wa kamati ya maandalizi Ustadhat Asmaa Raadu ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kwa utukufu wa Mwenyezi Mungu tumekamilisha maandalizi yote ya mkutao wa tatu wa waandishi wa habari, maandali haya yamefanyika kwa kipindi cha karibu miezi mitatu, na yamekamilika katika sekta nyingi, miongoni mwa sekta hizo ni:

  • 1- Tumefanya makubaliano na kamati ya elimu kwa ajili ya kujaji tafiti za habari zitakazo wasilishwa.
  • 2- Tumekubaliana na waandoshi wa jarida la Riyadhi Zaharaa, katika mkutano huu wa tatu waweke vipengele maalumu vinavyo endana na mkutano huu.
  • 3- Tumewaalika viongozi maarufu kitaifa wahudhurie katika mkutano huu.
  • 4- tumewasiliana na kituo cha Swidiqa Twahira (a.s) na kuwaomba wawe wenyeji wa mkutano, jambo litakalo wapa uhuru mkubwa wageni waalikwa”.

Naye raisi wa wahariri wa jarida la Riyadhi Zaharaa ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya maandalizi Ustadhat Laila Ibrahim Huru amesema kua: “Hakika mkutano wa waandishi wa habari hufanywa kila mwaka katika kuadhimisha kumbukumbu ya kuanzishwa kwa jarida la Riyadhu Zaharaa (a.s) lakini mkutano wa mwaka huu utakua na vipengele vingi, miongoni mwa vipengele hivyo ni:

  • 1- Mkutano kufanywa siku mbili mfululizo.
  • 2- Kutakua na kipengele cha kuwasilisha uzowefu wa waandishi wa jarida.
  • 3- Wageni watatembelea miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu kwa mfano, jengo la kibiashara la Afaaf na miradi mingine”.

Tunapenda kufahamisha kua mkutano huu ulianzishwa kwa ajili ya kushajihisha waandishi wa kike wa Atabatu Abbasiyya tukufu na kufikisha sauti ya wanahabari wa Zainabiyya kila pembe ya Dunia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: