Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu umetoa ufafanuzi kuhusu kufungwa sehemu ya haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wamebainisha kua kufungwa kwa sehemu ya haram tukufu –upande wa wanaume uliyopo katika mlango wa kibla na pembezoni mwake- kunatokana na kazi zinazo endelea hivi sasa za kuweka marumaru, kwa hiyo wanaume wanapitia sehemu ya wanawake ambayo imesha wekwa marumaru kwa muda hadi kazi itakapo kamilika, na wanawake wanapitia kwenye sardabu tukufu ambayo kimsingi imejengwa rasmi kwa ajili ya wanawake.
Atabatu Abbasiyya imeweka alama zinazo muongoza zaairu pamoja na kuweka watumishi kwa ajili ya kazi hiyo, uongozi mkuu umesema kua kazi inafanywa usiku na mchana kwa ajili ya kuhakikisha inakamilika kwa wakati na isilete usumbufu kwa mazuwaru watukufu.