Kamati ya maandalizi ya kongamano la jinai ya Spaika yalitaka bunge la Iraq kutunga sheria itakayo itambua siku ya (12 Juni) kua siku ya kumbukumbu ya mauaji ya halaiki kitaifa…

Maoni katika picha
Mjumbe wa kamati ya maandalizi ya kongamano la fatwa tukufu ya kujilinda linalo fanyika kwa mwaka wa tatu chini ya kauli mbiu isemayo: (Ushindi umetokana na nyine ni wenu na nyie ndio washindi) linano fanyika tarehe (14 hadi 15 Shawwal 1439h) sawa na (29 hadi 30 Juni 2018m) Shekh Abbasi Quraishi ametangaza maazimio yaliyo fikiwa katika kongamano la jinai ya Spaika, ifuatayo ni nakala ya maazimio hayo:

  • 1- Tunalitaka bunge la Iraq liunde sheria itakayo itambua siku ya tarehe (12 Juni) kua siku ya kumbukumbu ya mauwaji ya Spaika kitaifa.
  • 2- Kuunda kamati ya watalamu itakayo fatilia mauwaji ya Spaika na kuyaingiza katika orodha za mauwaji ya halaiki kimataifa.
  • 3- Kulipa kisasi kwa walio endesha mauwaji hayo.
  • 4- Kuhimiza wahusika wakamilishe kufukua makaburi ya pamoja ambayo yapo kumi na saba, yamesha fukuliwa kumi na tano bado mawili, jumla ya miili iliyo patikana ni elfu moja mia moja na hamsini na tatu, pia tunawataka wahusika wakabidhi miili ipatayo mia nne na arubaini kwa familia zao ambayo bado haija kabidhiwa hadi leo.
  • 5- Tunaomba litengwe eneo katika mji wa Najafu au Karbala tukufu na kulifanya makaburi na makumbusho, watakapo zikwa mashahidi hao, kila kabuli liandikwe jina la shahidi na kuwekwa picha yake pamoja na maelezo mafupi kuhusu shahidi na kila kinacho husiana na mauwaji ya Spaika, sambamba na kuweka vitu vya kumbukumbu likiwemo jiwe walilo chinjiwa juu yake.
  • 6- Kuwe na kongamano la kitaifa kila mwaka la kukumbuka tukio la mauwaji ya Spaika.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: