Mahafali ya Qur’an yahusisha mradi wa kiongozi wa wasomaji wa Qur’an na usomaji wa mashairi katika kuhitimisha ratiba ya siku ya kwanza ya kongamano la fatwa tukufu ya kujilinda…

Maoni katika picha
Mwishoni mwa ratiba ya siku ya kwanza ya kongamano la fatwa tukufu ya kujilinda linalo fanyika chini ya kauli mbiu isemayo: (Ushindi unatokana na nyie ni wenu na nyie ndio washindi) kuanzia tarehe (14 hadi 15 Shawwal 1439h) sawa na (29 hadi 30 Juni 2018m) vimefanyika visomo vya aina mbili:

Kwanza: Visomo vya Qur’an, na ikatangazwa kuanza kwa mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa, unao jihusisha na kuandaa wasomamji, unao fanywa kila mwaka na Maahadi ya Qur’an ya Atabatu Abbasiyya tukufu, Qur’an hiyo imesomwa na Muhammad Abbasi, kisha ukafuata ujumbe wa mkuu wa Maahadi ya Qur’an tukufu Shekh Jawaad Nasrawiy, ambaye alisisitiza umuhimu wa mradi huo, ambao ni miongoni mwa miradi muhimu ya Qur’an inayo simamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, unalenga kulea na kuandaa wasomaji wa Qur’an tukufu hapa Iraq, husimamiwa moja kwa moja na kuendeshwa na kituo cha kuandaa wasomaji na mahafidhu wa Qur’an katika Ataba tukufu, uzowefu wao umezaa mafanikio kila mwaka, baada ya hapo ikasomwa tena Qur’an na bwana Najmu Kaamil, halafu kipengele hicho kikahitimishwa na kisomo cha Ali Najmu..

Pili: Kisomo cha kaswida za kiiraq kutoka kwa washairi wa mikoa tofauti ya Iraq, ambao ni: kutoka Karbala mshairi Zainul-Aabidina Saidi, kisha mshairi Ghazwani Ghalibi kutoka katika mkoa wa Misaan, halafu akasoma Abbasi Abadi kutoka Nawsiriyya, kisha ukaingia wakati wa mkoa wa Baabil akasoma mshairi Maliki Sultani, kutoka mkoa wa Basra akasoma Murtadha Bahadeli, kisha akasoma tena mshairi kutoka Naswiriyya akasoma Ali Hassan Alwaan, na mwisho kabisa akasoma mshairi wa Karbala Alaa Zubaidi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: