Tume ya turathi za Karbala yafanya vikao vya kujadili athari za maadhimisho ya kidini katika kujenga uislamu…

Maoni katika picha
Miongoni mwa mambo yanayo pewa umuhimu mkubwa na harakati ya turathi za Karbala iliyo chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu, ambacho ni kituo kinacho tatua mambo ya kielimu kuhusu turathi za Karbala kufuatia kushajihisha utafiti wa kielimu na majadiliano yanayo jenga, kwa kukaribisha wataalamu walio bobea katika sekta hii, ili waweze kutoa mchango wao kila mmoja kutokana na uwezo wake kupitia vikao vya kujadiliana, hivi karibuni imewasilishwa maudhui isemayo: (Athari za maadhimisho ya kidini katika kujenga uislamu) ndio ilikua anuani ya kikao cha pili.

Muwasilishaji wa mada katika kikao hicho alikua ni Dokta Zainul-Aabidina Mussa Jafari kutoka katika chuo kikuu cha Karbaka, alianza kwa kuelezea uislamu katika mji mtukufu wa Karbala, na namna wakazi wa mji huo wanavyo watukuza watu wanaokuja kufanya ziara katika mji huu, ameuelezea uislamu katika mji wa Karbala kwa kuangalia sekta mbalimbali na mambo yaliyo tokea kihistoria, akabainisha nadhariya ya majengo na uhandisi katika mtazamo wa watu wa Magharibi na watu wa Mashariki, akatoa mifano ya majengo ya kiislamu na mabadiliko yanayo tokea katika kila zama.

Kikao hicho cha majadiliano kutokana na maudhui zilizo kua zimewasilishwa kilikua na michango mingi ya maoni pamoja na maswali kutoka kwa wahudhuriaji ambao miongoni mwao ni wasomi wa sekula walio bobea katika sekta ya turathi za Karbala, mtoa mada alitoa majibu na kufafanua pale alipo hitajika kutoa ufafanuzi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: