Familia za mashahidi walio tekwa waisifu Atabatu Abbasiyya tukufu kwa uwangalizi wake kwao kufuatia kutekwa kwa watoto wao na juhudi ilizo fanya za kutaka kuwaokoa…

Maoni katika picha
Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya zimetuma ujumbe mzito kwenda kutoa pole kwa familia za mashahidi walio tekwa na kuuwawa na magaidi wa Daesh hivi karibuni.

Ugeni huo umepokelewa na wake wa mashahidi pamoja na ndugu wa karibu, Atabatu Abbasiyya imewakilishwa na rais wa kitengo cha dini Shekh Swalahu Karbalai na jopo la watumisi wa kitengo hicho.

Jambo hili ni sehemu ya muendelezo wa juhudi nyingi zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, tangu kutekwa kwa watu hao imefanya kila iwezalo kwa ajili ya kutaka kuwakomboa, nalo ni jambo la kawaida kwake kwa ajili ya kuimarisha mapenzi na kuwapa pole na kusimama pamoja na kila mwenye matatizo hapa Iraq, pia kuimarisha uhusiano na Ataba zingine tukufu.

Familia za mashahidi walio tekwa zilionyesha shukrani zao kutokana na namna Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya zinavyo wajali na kuwathamini sana watu wa mkoa huu, hili sio jipya, wamefanya mambo mengi yasiyo weza kuhesabika, walitoa sifa sarmi jinsi Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya kiongozi wake mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi ambaye alikua mstari wa mbele katika kufuatilia jambo hili tangu siku za kwanza kabisa za kutekwa kwao, hakika alifuatilia swala hili kwa karibu sana, aliwasiliana na serikali ya eneo husika pamoja na kituo cha usalama kwa ajili ya kuwakomboa mateka hao lakini matokeo yake yamekua tofauti na tulivyo taka.

Mashahidi wetu watukufu wamekwenda kuungana na msafara wa mashahidi walio mwaga damu zao katika machinjo ya utukufu, kwa ajili ya kuhakikisha taifa hili linaendelea kua huru tena lenye utukufu na wala lisinajisiwe na magaidi wa Daesh.

Rais wa kitengo cha dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu Shekh Swalahu Karbalai ametuambia kua: “Tumepokea kwa machungu makubwa taafira ya kuuwawa kishahidi kwa watu watukufu miongoni mwa watoto wetu, walio kua na mchango mkubwa tangu ilipo tolewa fatwa tukufu ya kuilinda Iraq na Marjaa mkuu, walikua washirika muhimu katika kutoa misaada ya kimkakati kwa ndugu zao wapiganaji, Mwenyezi Mungu mtukufu amependa waungane na ndugu zao walio uwawa kwa ajili ya kulilita taifa hili, kuwepo kwetu hapa leo tumekuja kuwapa pongezi familia zao kutokana na ndugu zao kupata hadhi kubwa ya kua mashahidi, na kuwapa pole kwa kuondokewa na wapenzi wao na kuwataka wajiliwaze kupitia Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s), na tumewafikishia salamu na pole kutoka kwa viongozi wakuu wa Ataba mbili tukufu pamoja na watumishi wote wa Ataba hizo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: