Kwa namba: Haya ndiyo mafanikio ya Aprication (app) ya kwanza hapa Iraq (Aprication ya Haqiibatul-Mu-umin) baada ya miaka mitano ya kuanzishwa kwake…

Maoni katika picha
Kuna aina nyingi za Aprication katika simu za kisasa (smart phone) lakini ni chache zinazo kubalika na kupata mafanikio makubwa na kukidhi matakwa ya watumiaji, na kuendelea kutawala katika mawasiliano pamoja na kutatua tatizo lolote la kiufundi linalo weza kutokea, Aprication (App) ya Haqiibatul-Mu-umin) iliyo tengenezwa na idara ya intanet ya Atabatu Abbasiyya tukufu ni moja kati ya Aprication inayo fanya vizuri, Aprication hii inayo gusa nyoyo na akili za watu imeweza kutumia teknolojia ya kisasa na kumuwekea mkononi mtumiaji kila kitu kinacho hitajika na mu-umin katika nyanja ya ibada na zinginezo.

Aprication (App) ya Haqiibatul-Mu-umin ambayo ni miongoni mwa App za kiislamu imezizidi App nyingi za mfano wake kwa mujibu wa takwimu zifuatazo:

  • - Ni Aprication ya kwanza kupakuliwa na watu wengi zaidi hapa Iraq.
  • - Imepakuliwa na zaidi ya watu milioni tisa wanao itumia.
  • - Kuna watumiaji milioni moja walio hai kila mwezi.
  • - Kila mwezi inapakuliwa na watu laki tatu.
  • - Aprication hii imeenea sana katika nchi zingine duniani, inatumika katika zaidi ya nchi (146) kote duniani.
  • - Idadi ya swala za faradhi zilizo swaliwa kadha kupitia Apricatio hii zimefika (400,000,000) milioni mia nne.
  • - Idadi ya faradhi zilizo swaliwa kadha katika mwezi wa Ramadhani ulio pita zimefika milioni (35) sawa na zaidi ya swala milioni moja kila siku.
  • - Aprication hii inafanya kazi katika zaidi ya aina za simu (190) kutoka katika makampuni tofauti, hivyo imekubalika sana, tofauti na aina zingine ambazo huchagua aina za simu.

Kumbuka kua Aprication (App) hii inapatikana katika (Google Play) na katika ukurasa wa Aprication za mtandao wa kimataifa wa Alkafeel.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: