Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya zafanya majlisi ya kuomboleza mateka waliouwawa kishahidi…

Maoni katika picha
Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya zimefanya majlisi ya kuomboleza na kuwarehemu watu walio tekwa na kuuwawa na magaidi wa Daesh katika barabara ya (Bagdad/ Karkuuk), katika eneo lililo wekwa paa kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, na kuhudhuriwa na ndugu wa mashahidi pamoja na viongozi wa kidini na kijamii, na wawakilishi wa wapiganaji wa Hashdi Sha’abi na viongozi wa kikabila bila kuwasahau watumishi na viongozi wa Ataba mbili tukufu.

Bwana Fadhili Auzu ambaye bi mjumbe wa kamati kuu ya uongozi wa Atabatu Husseiniyya tukufu amebainisha kua: “Baada ya wananchi wa Iraq na wakazi wa Karbala kupata taarifa za kuuwawa kwa vijana watukufu walio itikia wito wa Marjaa dini mkuu wa jihadi ya kifaya (kufoshelezeana), watu walio fanya kazi kubwa ya kutoa misaada kwa wapiganaji, hakika mji umekua na huzuni kubwa kutokana na vilio vya watoto walio kuwa wakiomba kukombolewa kwa baba zao lakini vilio hivyo havikuzaa matunda, magaidi wamefanya haraka kuwauwa, kwa hiyo Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya wamefanya majlisi hii ya kuomboleza kwa majonzi makubwa sana yaliyo jaa katika nyoyo zetu, hakika wameuwawa kishahidi wako mbele ya Mwenyezi Mungu wanaruzukiwa”.

Akaongeza kusema kua: “Hakika magaidi wa Daesh wamejivua na ubinadamu na imekuwa kawaida yao kufanya hiyana na vitimbi, na wala hawatofautishi baina ya tabaka fulani na lingine, tukio la mwisho ni ushahidi mzuri juu ya hilo, Marjaa dini mkuu aliyasema haya katika khutuba ya Ijumaa, damu za watu wa Karbala zimechanganyika na damu za watu wa Ramadi katika tukio la kinyama, tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu awarehemu Mashahidi wa Iraq na awape subira watu wa familia zao”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: