Kituo cha elimu na ukuzaji wa vipaji Alkafeel chazindua App (Aprication) ya Siraji na chazitaka shule zote ziitumie…

Maoni katika picha
Katika muendelezo wa kutengeneza App, kituo cha Alkafeel cha elimu na kukuza vipaji kilicho chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu kimetangaza uzinduzi wa App ya Siraaj, inayosaidia kujenga mawasiliano baina ya shule na wazazi na inaongeza kiwango cha ushirikiano baina yao, inapunguza muda wa walimu na wazazi wa kufuatilia maendeleo ya mwanafunzi na inaendana na maendelea ya teknolojia ya sasa, pia ni kuyafanyia kazi maendeleo ya teknolojia kielimu na kimalezi hapa Iraq.

Mkuu wa kituo Ustadh Samiri Falahu Hassan Swafi ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Hakika Atabatu Abbasiyya tukufu imeanza kupiga hatua kubwa katika sekta ya kutengeneza App, inafanyia kazi kauli ya kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi isemayo: (Tunaanzia walipo ishia wengine), App (Apricatio) hii ni moja ya App nyingi zilizo buniwa, kusanifiwa na kutengenezwa pamoja na kuziingiza katika matumizi kwa ubora unao endana na viwango vya ubora vya sekta hii, tena kwa kutumia wataalamu wake bila kutegemea mtaalamu yeyote wa nnje, App hii imeleta mabadiliko katika sekta ya elimu na malezi (tulichukua maoni kutoka kwa watu wenye uzowefu pamoja na walimu), hii ni mara ya kwanza kuingia katika matumizi, imebuniwa na kupangiliwa na vijana wa kiiraq na imeonyesha mafanikio makubwa (App ya Siraji: inahuduma nyungi za kielimu, na ni rahisi kuitumia)”.

Akaongeza kua: “App ya Siraji imeleta mwamko katika sekta ya elimu na malezi, imetengenezwa baada ya uchunguzi wa kina na kuchambua maoni na ushauri mwingi kutoka kwa watafiti walio bobea katika sekta hii, ili kuifanya kua bora zaidi kimpangilio”.

Akabainisha kua: “App hii imetangazwa rasmi katika maonyesho tuliyo shiriki hivi karibuni baada ya kuonyesha mafanikio katika majaribia mengi yaliyo fanyika, wazazi na walimu wote wamethibitisha ubora wake”.

Ustadh Samiri akatoa wito: “Kwa shule zote za msingi na sekondari watumie App hii ambayo itawaondolea vikwazo vya mawasiliano na itachangia kwa kiasi kikubwa kuleta maendeleo mazuri kwa wanafunzi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: