Kukamilika kwa ratiba ya kwanza ya hema za Skaut za Alkafeel kwa wanafunzi wa sekondari…

Maoni katika picha
Idara ya mahusiano na vyuo vikuu kupitia ofisi ya harakati za shule katika Atabatu Abbasiyya tukufu imekamilisha ratiba ya kwanza ya hema za Skaut kwa wanafunzi wa sekondari, ambayo limeshiriki kundi kubwa la watoto wa mashahidi wa wanajeshi na Hashdi Sha’bi pamoja na makundi mengine, kwa ajili ya kukuza uwezo na vipaji vya wanafunzi na kuwapa mwongozo sahihi wa kimazingira na kielimu, hilo ni miongoni mwa matokea ya mafanikio mazuri yanayo patikana katika ratiba hii, uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu umejitolea kufadhili mradi huu, ambao ni miongoni mwa harakati za idara ya mahusiano na vyuo vikuu na ipo katika mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel.

Hafla ya kufunga imefanywa ndani ya ukumbi wa jengo la Shekh Kuleini (q.s) baada ya Qur’an ya ufunguzi na kusomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, kulikua na ujumbe wa Atabatu Abbasiyya ulio wasilishwa na Abdulsataar Hajami, miongoni mwa aliyo sema ni: “Kama ilivyo tuahidi Atabatu Abbasiyya tukufu kuhusu kufanya makongamano na program za kujenga uwezo na kuibua vipaji, imefanyika program hii chini ya anuani isemayo; hema za makamanda wa Alkafeel, tulitaka kutumia muda mrefu zaidi ambao ungetuwezesha kufundisha mambo mengi, lakini muda sio rafiki kwetu, kwa hiyo tumetumia kanuni ya kifiqhi isemayo (hautaacha jambo jepesi kwa sababu ya zito)”.

Akaongeza kua: “Natarajia na napenda kuwaona mnakua sawa na anuani yenu inayo sema (makamanda wa Alkafeel), muwe na ushujaa, nguvu na msimamo katika kuinusuru dini na haki, natarajia mkamilishe kazi iliyo anzwa na wazazi wenu ya kujitolea na kupambana kwa ajili ya kulinda dini na heshima dhidi ya magaidi wa Daesh”.

Hafla hiyo ilipampwa na igizo lililo fanywa na wanafunzi walio shiriki katika mafunzo ya hema hizo, hafla ikahitimishwa kwa kugawa vyeti vya ushiriki kwa wanafunzi hao walio onyesha furaha na shukrani kubwa kwa Atabatu Abbasiyya kwa kuwafanyia jambo hili tukufu, wakasisitiza kua wamenufaika sana na mihadhara waliyo pewa, hususan pale wanapo ona mabadiliko makubwa ya namna wanavyo amiliana na marafiki zao pamoja na watu wengine, hili ndio linalo lengwa na wafadhili pamoja na wasimamizi wa hema hizi tukufu..

Kumbuka kua hema hizi zimejumuisha harakati za dini na elimu kwa kuwa na vipengele vya kielimu, kitamaduni na kimichezo, ambapo kulikua na mihadhara mbalimbali pamoja na masomo ya maarifa ya Qur’an sambamba na mihadhara ya maendeleo ya kibinadamu, na mingine inayo fafanua ulimwengu wa wanafunzi, masomo yalikuwepo ya nadhariyya na vitendo pamoja na mashindano ya vipengele vya kidini na kimichezo (CPR) inayo burudisha moyo, pia kulikua na maswali ya kifiqhi, kiitikadi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: