Kifo cha Abulfadhil Abbasi (a.s) kimefanana na cha ammi yake Jafari bun Abu Twalibu (a.s) kwa kukatwa mkono wake wa kulia kisha wa kushoto kabla ya kuuwawa kwake, lakini alimshinda ammi yake kwa kupigwa na chuma kichwani kwake, na wakaukata mwili wake vipande vipande, Imamu Zainul-Aabidina Ali bun Hussein Sajjaad (a.s) alikua analia kila anapo mkumbuka Ammi yake Abbasi (a.s) na akimkumbuka ammi yake Jafari bun Abu Twalib (a.s) analia pia.
Siku moja –kama ilivyo kuja katika kitabu cha Aamali Swaduqu kutoka kwa Abu Hamza Shimali- alimwangalia (a.s) Abdullahi bun Abbasi bun Amirulmu-uminina (a.s), akakumbuka kisha akasema: ((Hakuna siku ngumu kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) kama siku aliyo uwawa ammi yake Hamza bun Abu Twalib simba wa Mwenyezi Mungu na simba wa Mtume wake, kisha siku ya vita ya Mu-uta aliyo uwawa mtoto wa ammi yake Jafari bun Abu Twalib (a.s), wala hakuna siku ngumu kama siku aliyo uwawa Hussein, alizungukwa na watu elfu thelathini wanao dai kua ni katika umma huu, kila mmoja anajikurubisha kwa Mwenyezi Mungu kwa kumwaga damu yake (damu ya Hussein), wakati yeye anawakumbusha kuhusu Mwenyezi Mungu hawakuwaidhika hadi wakamuua kwa chuki, dhulma na uwadui)). Kisha akasema: ((Mwenyezi Mungu amrehemu ammi yangu Abbasi, alipambana akajitolea kumlinda ndugu yake kwa nafsi yake hadi akakatwa mikono yake, Mwenyezi Mungu akambadilishia kwa kumpa mbawa mbili anaruka pamoja na Malaika peponi kama alivyo fanya kwa Jafari bun Abu Twalib (a.s), hakika Abbasi mbele ya Mwenyezi Mungu mtukufu anahadhi kubwa atawashinda mashahidi wote siku ya kiyama)).
Hakika neno (wote) katika kauli ya Imamu Zainul-Aabidina (a.s) (Atawashinda mashahidi wote) ni neno la jumla na enevu, linakusanya na wasio kua maasumina wote hata Hamza bun Abdulmutwalib na Jafari bun Abu Twalib, hakika hao wote wako chini ya Abbasi bun Ali (a.s) kwa utukufu na nafasi yake mbele ya Mwenyezi Mungu siku ya kiyama, kapata utukufu huo kutokana na ukubwa wa balaa alilo kumbana nalo na ukubwa wa mitihani yake, na ukubwa wa msiba wake, jeshi la Bani Umayya lilimuuwa vibaya mno katika ardhi ya Karbala na wakasulubu mwili wake akiwa bado yu hai, kutokana na chuki zao kwake, na kulipa kisasi cha ushujaa wake na nguvu zake.
Kutokana na ugumu wa roho zao na chuki zao hawakutosheka na kumuua peke yake, walimkata mkono wa kulia na wakushote, wakakata na mguu wake wa kulia na wakushoto, wakaponda kichwa chake kwa chuma kizito, na wakamkata vipande vipande, wakamchoma mikuki mingi katika mwili wake ikasimama kama manyoya ya nungunungu, amani iwe juu yake siku aliyo zaliwa na siku aliyo uwawa kishahidi katika njia ya Mwenyezi Mungu na siku atakayo fufuliwa na kua hai.