Kukamilika kwa ukarabati wa mfumo mkuu wa viyoyozi katika Atabatu Abbasiyya tukufu…

Maoni katika picha
Kutokana na kuongezeka kwa joto na kuwepo kwa haja ya kutumika viyoyozi (AC) ndani ya eneo lote la haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na kujikinga na tatizo lolote linalo weza kupelekea kuzimika ghafla kwa viyoyozi hivyo, idara ya viyoyozi chini ya kitengo cha uangalizi wa kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya kazi ya kukarabati mfumo wote wa viyoyozi ndani ya Ataba tukufu, hasa katika uwanja wa haramu na ndani ya haramu yenyewe sambamba na kumbi za chini (sardabu) zote, pamoja na kuweka njia mbadala iwapo likitokea tatizo lolote litakalo pelekea kuzimika kwa viyoyozi (Allah atuepushie).

Kwa mujibu wa maelezo ya watendaji wa kazi hiyo, vimefanyiwa matengenezo vifaa vyote vya viyoyozi pamoja na mabomba yake ya njia ndogo na kubwa, pamoja na mfumo wa umeme unao tumika kwenye viyoyozi, sehemu zote za maunganisho zimetengenezwa vizuri, pia umetengenezwa mfumo maalumu utakao wezesha viyoyozi vya upande wa mgahawa (mudhifu) wa Abulfadhil Abbasi (a.s) kufanya kazi muda wote, pamoja na kuyafunika mabomba yake.

Kumbuka kua kitengo cha usimamizi wa kihandisi cha Atabatu Abbasiyya ni miongoni mwa vitengo muhimu, na kina idara nyingi, kina mafundi na wahandisi wengi wanao fanya kazi muda wote katika maeneo yote ya Ataba tukufu, pamoja na kazi za ukarabati wamesha tekeleza miradi mingi mikubwa na midogo, kazi hii ya ukarabati wa mfumo wa viyoyozi vya Atabatu Abbasiyya tukufu imefanywa na mafundi wa kitengo hicho bila msaada wowote wa mafundi wa nje.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: