Baada ya kuteua watu watakao fuatana na misafara ya mahujaji mwaka huu, kutoka kitengo cha dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu, wameshiriki katika mkutano ambao hufanywa kila mwaka wa waongozaji wa misafara ya mahujaji katika nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu, mkutano huo umesimamiwa na ofisi kuu ya maelekezo na utafiti chini ya kamati kuu ya hijja na umra kwa kusaidiana na kitengo cha dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu, na umefanyika katika jengo la Imamu Hassan Almujtaba (a.s) ndani ya malalo ya Imamu Ali (a.s).
Shekh Ali Mujaan mmoja wa waongozaji kutoka katika kitengo cha dini ambaye amehudhuria mkutano huo amesema kua: “Hakika mkutano umekua na mahudhurio makubwa ya waongozaji wakiume na wakike wanaotarajia kufuatana na misafara ya wairaq wanaokwenda hijja, ulihudhuriwa pia na Mheshimiwa Ayatullahi Shekh Muhammad Baaqir Airuwani pamoja na rais wa kamati ya hijja Dokta Khalidi Atwiyya ambaye katika ujumbe wake alibainisha nafasi muhimu aliyo nayo muongozaji wa msafara wa hijja katika kutekeleza ibada ya hiyo, inategemea juhudi zao na utekelezaji bora wa ibada ukizingatia kua wao ndio tegemeo la kufanikiwa kwa kamati ya hijja, akabainisha majukumu makubwa waliyo nayo ya kutoa mafunzo sahihi kwa mahujaji, kwa mujibu wa mafundisho ya kifiqhi na sheria ya kiislamu ya namna ya kutekeleza ibada ya hijja”.
Akaongeza kua: “Kulikua pia na ujumbe elekezi kutoka kwa Ayatullahi Shekh Muhammad Baaqir Airuwani ambaye alibainisha nafasi ya muelekezaji wa mahujaji, akawahimiza kuongeza juhudi kwa ajili ya kufanikisha ibada hiyo tukufu”.