Kuanza maandalizi ya kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada la kumi na tano la mwaka (2019m-1440h)…

Maoni katika picha
Baada ya wajumbe wa kamati ya maandalizi ya kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada kumtembelea Imamu wa nane Ali bun Mussa Ridhwa (a.s), ujumbe huo umewatembelea baadhi ya mashekhe wakubwa katika mji mtukufu wa Mashhadi, kwenda kuwashukuru kwa michango yao iliyo pelekea kufanikiwa kwa kongamano, walianza kwa kumtembelea Alammah Sayyid Muhammad Ali Shirazi, ambaye alisifu uendeshwaji wa kongamano na akaonyesha kufurahishwa zaidi na wingi wa washiriki kama alivyo ona kupitia vyombo vya habari –kwa mujibu wa mameno yake- akaishukuru na kuiombea dua kamati ya maandalizi iendelee kua imara na kupata mafanikio.

Baada ya hapo ujumbe huo ulimtembelea Alammah Sayyid Shahri Stani ambaye ni kiongozi mkuu wa taasisi ya Ahlulbait (a.s), baada ya kupewa maelezo kwa ufupi kuhusu kongamano lililo pita na mambo yanayo tarajiwa kuongezwa katika kongamano lijalo, ikiwemo mashindano ya uandishi wa vitabu, na uandishi wa vitabu vya mashairi, Sayyid Shahri Stani amesema kua: “Kongamano la mwaka huu la awamu ya kumi na nne lilikua zuri kushinda makongamano ya nyuma kutokana na uzowefu mkubwa ambao mmesha pata”, akasifu nukta moja muhimu ambayo ni “Uwepo wa washiriki kutoka dini tofauti na madhehebu tofauti na watu wa tabaka tofauti, kana kwamba ni uwa lenye harufu nzuri lililopo katika sahani la Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s)”, akasisitiza umuhimu wa kutoa kipawa mbele cha vikao vya pembezoni baina ya wageni, hakika vikao hivyo vina umuhimu mkubwa katika ratiba ya kongamano, tena vinafaida kubwa zaidi”, mwisho wa nasaha zake alimuomba Mwenyezi Mungu mtukufu awape nguvu watendaji wa Ataba tukufu.

Kumbuka kua kamati hiyo ya maandalizi ilishiriki kushindikiza jeneza na kusoma dua ya marehem Alammah Sayyid Ahmadi Khatamiy na mzazi wa Alammah Sayyid Muhsin Khatamiy, na uliongozwa na katibu mkuu wa Atabatu Husseiniyya tukufu Sayyid Jafari Mussawi, kutokana na maelezo ya Ustadh Jawadi Hassanawi ambaye ni mjumbe wa kamati ya maandalizi: “Kutokana na maelekezo ya viongozi wakuu wa kisheria wa Ataba mbili tukufu ya kuanza mapema maandalizi ya kongamano la kumi na tano, tumefanya ziara hii kwa ajili ya kubadilishana fikra na kusikiliza maoni ya watu wengine pamoja na kunufaika na uzowefu wa miaka ya nyuma”.

Fahamu kua Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya hufanya kongamano hilo kila mwaka kwa ajili ya kuadhimisha kuzaliwa kwa miezi ya Muhammadiyya kuanzia tarehe (3-7 Shabani), huambatana na vipengele vingi muhimu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: