Atabatu Abbasiyya tukufu yapokea wanafunzi wanao jiandaa na mitahani ya mwisho wa mwaka na yawaandalia mazingira bora ya kujisomea…

Maoni katika picha
Kutokana na kuongezeka kwa joto na kukatika katika kwa umeme sehemu nyingi za mji, pia kufuatia kukaribia kwa mitihani ya mwisho wa mwaka ya wanafunzi wa darasa la sita, Atabatu Abbasiyya tukufu imefungua milango kwa wanafunzi hao wanao jiandaa na mitihani ya mwisho wa mwaka kuja kujisomea, kwani hiki ni kipindi muhimu sana katika maisha yao kwani ndicho kinaamua mustaqbali wao.

Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu umeagiza kuandaliwa maneo maalumu kwa ajili yao na kuweka kila kinacho hitajika kwa ajili ya kuwawezesha kujikumbusha masomo yao, kuanzia asubuhi Ataba tukufu inapokea makumi ya wanafunzi, miongoni mwao kuna wanao kaa katika kumbi za chini (sardabu) na wengine wanakaa katika korido za haram tukufu, wengine wanakaa ndani ya maktaba ya Ataba tukufu na wengine wanakaa katika uwanja wa haram tukufu, wana uhuru wa kukaa popote miongoni mwa sehemu hizo, kila kitu kinacho hitajika kipo, kama vile maji baridi ya kunywa, mwanga wa kutosha na viyoyozi muda wote, sehemu zote zimeandaliwa vizuri kwa kujisomea, uwepo wao katika eneo hili tukufu na kujisomea kwa pamoja kuna umuhimu mkubwa na kunawapa matumaini wa kufanya vizuri katika mitihani yao.

Wanafunzi wamesema kua mazingira ya kujisomea katika Ataba tukufu yanatofauti kubwa na mazingira ya kujisomea nyumbani au katika bustani za umma ambazo baadhi ya wanafunzi huwenda huko kujisomea, inatokana na maandalizi mazuri yaliyo fanywa na Ataba tukufu kwa ajili ya wanafunzi na mazuwaru pamoja na huduma zinazo tolewa, hakika mazingira haya yanamsaidia mwanafunzi kujikita katika masomo na kuhifadhi somo kwa urahisi katika kujiandaa na mtihani wa mwisho, hali kadhalika mazingira haya yanatuweka karibu na Abulfadhil Abbasi (a.s) na tunapata matumaini ya kufaulu na kufanikiwa kutokana na utukufu wake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: