Kamati inayo husika na kuandika kitabu kinacho elezea maandamano ya Shaabaniyya imetangaza kua hatua ya kwanza inamaendeleo makubwa, nacho ni miongoni mwa vitabu muhimu vinavyo andikwa na kituo cha (Amidi duwaliyyu lilbuhuthi wa dirasaat) cha Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kitengo cha mausuaat (vitabu) vya kielimu.
Kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa kitengo na msimamizi wa mradi huo Dokta Karim Hussein Naaswih alipo kutana na wajumbe wa kamati ya watafiti wanao tekeleza mradi huo, akaongeza kua: “Kwa uhudhuriaji wa wajumbe wa kamati na ugeni kutoka taasisi ya Shuhadaau (mashahidi) wanao wakilisha kituo cha kitaifa cha kuthibitisha jinai za utawala wa Ba’athi; tumefanya kikao kikubwa kwa lendo la kuwapa wajumbe taarifa muhimu zitakazo wasaidia katika uwandishi wao, katika kikao hicho yamejadiliwa mambo mengi, miongoni mwa mambo hayo ni: namna ya kuandika utangulizi, pamoja na kuthibitisha taarifa na kufanya mahojiano”.
Dokta Fuaad Twaariq Kaadhim mmoja wa wajumbe wa kamati ya watafiti wanao andika kitabu hicho amesema kua: “Katika kikao hiki tumepata mambo muhimu, miongoni mwa mambo hayo ni: Kuwa na uhakika wa yale tutakayo yaandika katika utangulizi wa kitabu, mambo yanayo husu hali halisi ya Iraq kwa ujumla kabla ya maadamano na yaliyo tokea wakati wa maandamano, na kugusia mambo muhimu ambayo tuliyajadili katika mikutano ya nyuma, pia tulijadili kuhusu kuandika kwa milango (sehemu), tayali tumesha pokea sehemu ya kwanza kutoka katika mikoa mingi, na mikoa mingine wameanza kuandika sehemu ya pili, na wamesha piga hatua kubwa, tumejadili pia kuhusu kuhakikisha ushahidi na kufanya mahojiano pamoja na namna ya kuyaingiza katika kitabu”.
Yametolewa maoni mbalimbali kutoka kwa watafiti pamoja na kuelezea mahitaji yao, yakajadiliwa kwa kina kwa ajili ya kuhakikisha wanatoa kitabu kinacho endana na mazingira halisi ya maandamano ya Shaabaniyya, pia waliwasilisha mambo yanayo husiana na viongozi wa juu na kuangalia nukta wanazo shirikiana zenye athari katika kufanikisha uandishi wa kitabu hiki.
Kumbuka kua maandamano ya Shaabaniyya yanayo julikana kama maandamano ya Machi 1991m, ni moja ya matukio muhimu katika historia ya Iraq, wananchi wa Iraq walifanya maandamano ya kishujaa dhidi ya dhulma walizo kuwa wakifanyiwa na utawala wa Ba’athi wa zama hizo.