Atabatu Abbasiyya yasaidia mradi wa kulea mayatima wa fatwa tukufu ya kujilinda…

Sehemu ya msaada unao tolewa na Atabatu Abbasiyya
Tangu kutolewa kwa fatwa tukufu ya kujilinda Atabatu Abbasiyya imeendelea kua mmoja wa wafadhili wakubwa, imekua ikitoa misaada ya aina mbalimbali inayo endana na maelekezo ya Marjaa dini mkuu yanayo himiza jambo hilo, bado inaendelea na mwenendo huo, imepiga hatua kubwa katika kuwalea mayatima na watoto wa mashahidi wa fatwa hiyo tukufu, ambayo kutokana na fatwa hiyo wananchi wa Iraq wameneemeka kwa kupata amani na usalama, na taasisi ya Fadhil inayo lea mayatima wa fatwa tukufu ya kujilinda ni mfano hai wa misaada inayo toa, kupitia mpango wa kusaidia unao itwa (Alkafeel ni baba yangu: chakula, tiba na mavazi).

Kuhusu misaada inayo tolewa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa taasisi hiyo, Shekh Hussein Turabi ambaye ni kiongozi wa taasisi hiyo ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Mradi wa (Alkafeel ni baba yangu: chakula, tiba na mavazi) ni mradi wa kibinadamu unao endeshwa na taasisi kwa lengo la kutoa maisha mazuri kwa familia za mashahidi wa fatwa tukufu ya kujilinda, kwa njia ya kuhusisha misaada ya kijamii, Atabatu Abbasiyya tukufu kufuatia maelekezo ya moja kwa moja kutoka kwa kiongozi wake mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi imekua msaada mkubwa katika kuendeleza mradi huu, ambao unaendana na mpango wa Ataba tukufu wa kusaidia sekta hiyo”.

Akabainisha kua: “Hakika mradi huu unasaidia yatima mmoja mmoja, baada ya yatima kuingizwa katika mradi taasisi hutoa vitambulisho vitatu kwa familia inayo ishi na yatima huyo, ambavyo vitainufaisha familia hiyo kwa mambo yafuatayo:

Kwanza: Kitanbulisho cha chakula: huiwezesha familia kuandaa mahitaji ya chakula, na kwends kutembelea maduka ya Nurul-Kafeel ambayo yako chini ya Atabatu Abbasiyya moja kwa moja na kuchukua mahitaji yao.

Pili: Kitambulisho cha tiba: kinawawezesha kupata matibabu bure katika kipindi chote ambacho yatima yupo chini ya usimamizi wa taasisi, taasisi ya Fadhil imefanya makubaliano na hospitali kadhaa ikiwemo hospitali ya rufaa Alkafeel ambayo ipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, ya kutoa aina zote za matibabu kwa mayatima hao, fahamu kua watu wanao pata matibabu hayo bila malipo ni pamoja na mke wa shahidi, mama, na watoto wa shahidi.

Tatu: Kitambulisho cha mavazi: Nalo ni jambo ambalo hutia furaha sana katika nyoyo za watoto, hununuliwa nguo mpya katika sikukuu na siku za matukio maalumu kupitia kitambulisho hicho, kwa kutumia kitambulisho hicho familia inaweza kutembelea maduka kadhaa ya nguo na kuchukua nguo wanazo taka, kitambulisho hicho kinajadidishwa (kinatiwa upya) kila baada ya miezi sita, kituo cha kibiashara cha Afaaf kina nafasi kubwa katika swala hili la mavazi”.

Akafafanua kua: “Pamoja na tuliyo sema; hakika Atabatu Abbasiyya tukufu ina nafasi muhimu ya kuwatia furaha mayatima kwa kuwaandalia safari za kitalii na ziara za Ataba mbalimbali pamoja na mambo mengine yanayo saidia kuwapunguzia unyonge”.

Kumbuka kua yoto haya ni muendelezo wa mambo mengi yanayo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa familia hizi tukufu, hii inatokana na kujitolea kwao, na haya yote ni kwa ajili ya kuwafanya wachanganyike na kuishi sawa na watu wengine katika jamii, na kuwafanya wasiishi katika mazingira ya unyonge ambayo mayatima hujihisi kutokana na uyatima wao.

Kwa ajili ya kuwasiliana na taasisi tajwa unaweza kutuma Email kupitia anuani ifuatayo: alfadael.fondation@gmail.com au piga simu namba: (07718466503 au 07601608978).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: