Atabatu Abbasiyya tukufu yaandaa na kuendesha semina kwa mabinti…

Maoni katika picha
Kwa ajili ya kuchangia katika malezi ya mabinti na kuwajenga kifikra na kielimu, idara ya wahadhiri wa kike ya Atabatu Abbasiyya tukufu inaendesha mafunzo kwa mabinti wenye umri wa miaka tisa hadi kumi na nane, kwa kufuata ratiba ya masomo iliyo andaliwa na kamati ya wabobezi, yenye masomo yanayo endana na umri wa washiriki, yanayo wasilishwa kwa njia bora kabisa ya kuzungumzisha akili zao na yanayo endana na mazingira yao halisi.

Makamo mkuu wa kitengo Ustadhat Taghridi Abdul-Khaaliq Tamimi ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Tumeandaa semina hii kwa ajili ya kunufaika na kipindi cha likizo za kiangazi na kuhakikisha wanakitumia vizuri kipindi hiki, tulitangaza kwa muda sasa, na tumeweka masomo maalumu kwa kila rika, baada ya kuwagawa katika makundi chini ya usimamizi wa wakufunzi wao, na kuna mwitikio mkubwa”.

Akaongeza kua: “Ratiba ina vipengele vingi, miongoni mwa vipengele muhimu ni:

  • - Masomo na mihadhara kwa namna ya kisomo duwara.
  • - Kisomo sahihi cha Qur’an pamoja na vipande vya tafsiri za baadhi ya aya zikishereheshwa kwa Qur’an na hadithi za mtume.
  • - Masomo ya historia za Maimamu wa Ahlulbait (a.s) na kuangalia hadithi zao na kuzilinganisha na mazingira halisi tunayo ishi hivi sasa.
  • - Masomo ya Fiqhi na Aqida yanayo endana na rika zao.
  • - Kuwafundisha fani ya ushairi na uzungumzaji.
  • - Kusoma mambo mengine mbalimbali”.

Akabainisha kua: “Masomo yanaendelea kila siku katika sardabu ya Imamu Kaadhim (a.s), Atabatu Abbasiyya imejitolea magari yanayo kwenda kuwachukua wanafunzi na kuwarudisha majumbani kwao kila siku”.

Tamimi akasisitiza kua: “Mwisho wa semina hii tutafanya hafla na kutoa vyeti pamoja na zawadi za kutabaruku kutoka katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na kuwashika mkono wanafunzi watakao fanya vizuri katika semina kwa kuendelea kuwasimamia katika masomo yao”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: