Kumbukumbu iumizayo: Kifo cha Imamu Swadiq (a.s)…

Maoni katika picha
Katika siku kama ya leo mwezi ishirini na tano Shawwal mwaka wa (148) hijiriyya, watu wa nyumba ya Mtume (a.s) na wapenzi wao walipata majonzi makubwa sana kutokana na kifo cha Imamu Jafari bun Muhammad Swadiq (a.s), Imamu wa sita katika Maimamu watakasifu wa nyumba ya Mtume walio bashiriwa na Mtume (s.a.w.w), babu yake ni Imamu Ali bun Hussein Zainul-Aabidina (a.s), amelelewa na baba yake Imamu Muhammad Baaqir (a.s), na amesoma kwake elimu ya Aqida, Sheria za kiislamu na maarifa ya dini tukufu, inasemekana kua aliishi na babu yake Ali bun Hussein miaka kumi na mbili, na akaishi na baba yake baada ya kifo cha babu yake miaka kumi na tisa na akaishi baada ya baba yake miaka thelathini na nne.

Kifa cha Imamu Swadiq (a.s) kilikua tukio kubwa lililo huzunisha ulimwengu wa kiislamu wa zama zile, watu walihuzunika kila sehemu, sauti za vilio zilisikika kila mahala, watu walikusanyika katika nyumba ya Imamu wakibubujikwa machozi kwa kuondokewa na mtu aliye kuwa kimbilio la waislamu wote.

Riwaya zenye nguvu zinasema kua Abu Abbasi Saffaah ambaye ni khalifa wa kwanza wa utawala wa bani Abbasi, alimtaka Imamu (a.s) aondoke Madina na kwenda Iraq, lakini aliamua kumuacha huru na akamruhusu kurudi Madina baada ya kuona miujiza mikubwa na tabia tukufu za Imamu (a.s).

Utawala ulipo fika kwa Mansuur Dawaniqi -ndugu wa Saffaah- akaangalia wingi wa wafuasi wa Imamu Swadiq (a.s), aliamua kumwita Iraq, na alikusudia kumuuwa zaidi ya mara tano, lakini kila mara aliahirisha baada ya kuona miujiza mikubwa kutoka kwa Imamu (a.s).

Mitihani ilifululiza kwa mjukuu wa Mtume Imamu Swadiq (a.s) katika zama za Mansuur Dawaniqi, alishuhudia mitihani mikubwa waliyo pitia Alawiyyiina na wafuasi wao sambamba na mambo aliyo kua akifanyiwa yeye binafsi, kiongozi muovu huyo alikua anamwita kila wakati, anamtukana na kumtisha wala alikua haheshimu hadhi, elimu na uchamungu wake, lakini pia muovu huyo hakutosheka na kumtukana Imamu pekeyake, bali alimuona Imamu ni tishio kwake..

Mansuur alikusudia kumuua bila kujali yatakayo tokea, akampa sumu kali mmoja wa watumishi wake ili amuwekee Imamu katika chakula, Imamu (a.s) akala chakula chenye sumu, akaanza kusikia maumivu makali mno, akafahamu kua mwisho wa uhai wake umekaribia na mauti yakaja haraka kwa mjukuu wa Mtume (s.a.w.w), wakati wa mwisho wa uhai wake akaanza kuhusia watu wa nyumbani kwake washikamane na tabia njema, na akawatahadharisha kukiuka amri za Mwenyezi Mungu na hukumu zake, akawa anasoma sura za Qur’an tukufu, kisha akamtazama jicho la mwisho mwanae Imamu Mussa Alkaadhim (a.s) na akakata roho mwezi (25 Shawwal 148h).

Imamu Mussa Alkaadhim (a.s) akamuandaa baba yake, akamuosha na kumvisha sanda, alimvisha nguo mbili alizo kua akifanyia Ihraam na kanzu pamoja na kilemba cha babu yake Imamu Zainul-Aabidina (a.s), na akamfunga shuka aliyo nunua Imamu Mussa Alkaadhim (a.s) kwa thamani ya dinari arubaini. Baada ya kumaliza kumuandaa Imamu Alkaadhim akamswalia pamoja na mamia wa waislamu.

Kisha wakabeba mwili wake mtukufu kwa ncha za vidole huku wakisoma takbira kwa wingi na watu wanalia sana, wanakumbuka utukufu wa Imamu na familia yake kwa umma huu, watu wenye elimu kubwa katika kila kitu. Mwili wake ukapelekwa hadi katika makaburi ya Baqii, akazikwa karibu na babu yake Imamu Zainul-Aabidina pamoja na baba yake Imamu Muhammad Baaqir (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: