Atabatu Abbasiyya tukufu yafanya majlis ya kuomboleza kifo cha Imamu Jafari Swadiq (a.s)…

Maoni katika picha
Miongoni mwa ratiba ya kuhuisha kifo cha Imamu wa sita katika Maimamu wa nyumba ya Mtume (a.s) Imamu Jafari Swadiq (a.s), Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya majlis zitakazo dumu siku mbili ndani ya ukumbi wa utawala katika haram tukufu na kuhudhuriwa na idadi kubwa ya watumishi na mazuwaru.

Muhadhiri wa majlis ni Shekh Swalahu Karbalai ambaye ni rais wa kitengo cha dini, ameelezea nyanja mbalimbali za maisha ya Imamu Jafari (a.s), pamoja na mambo mengine kuhusu Imamu Jafari (a.s), sambamba na kuelezea mazingira yaliyo msaidia kwa kiasi fulani kufundisha misingi ya dini ya kiislamu na mafundisho ya Ahlulbait (a.s), na aliendelea vipi baada ya baba yake (a.s) katika kipindi cha Uimamu wake uliodumu miaka thelathini na nne kulea vizazi vya wanachuoni na mafaqihi wema chini ya mwenendo wa Ahlulbait (a.s), katika hicho kipindi kigumu cha kisiasa alifanikiwa kuilinda madhehebu ya Ahlulbait (a.s).

Majlis ilihitimishwa kwa kusoma kaswida za kuomboleza zilizo amsha hisia za huzuni kutokana na tukio hili chungu, ambalo ni miongoni mwa matukio yaliyo uumiza sana umma wa kiislamu zama zile, umma ulijaa simanzi, sauti za vilio zilisikika katika nyumba za Hasimiyyiina na zinginezo, watu walijaa katika nyumba ya Imamu wakibubujikwa machozi kutokana na kifo cha mtu aliye kua ndio kimbilio la waislamu wote.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: