Macho yanalia yameloa machozi… yanamlilia mtukufu aliyopo Baqii Gharqad.
Macho yanalia machozi ya damu kwa kumkosa mtukufu… katika Aali Muhammad mfano wake haujapatikana.
Jicho gani lisilotoa machozi yake… kwa ajili ya kuhuzunika na kumlilia Jafari bun Muhammad.
Watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) waomboleza tukio lililo umiza umma wa kiislamu na watu wa nyumba ya mtume (a.s), lililo tokea siku kama ya leo mwezi ishirini na tano Shawwal mwaka wa (148h), la kuuawa kwa Imamu wa sita na mrithi wa elimu ya Manabii na Mitume aliye kufa kwa sumu Jafari bun Muhammad Swadiq (a.s).
Kama kawaida ya kumbukumbu hizi za majonzi, watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu baada ya Adhuhuri ya leo, wamefanya matembezi maalumu ya kukumbuka kifo cha Imamu Jafari Swadiq (a.s), na kwenda kumpa pole babu yake Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), jambo hili limekua mazowea hufanywa kila mwaka na watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu.
Waombolezaji walikusanyika katika uwanja wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na wakasimama kwa vikundi, kisha wakaanza kutembea kuelekea katika kaburi la Abu Abdillahi Hussein (a.s) huku wanaimba kaswida za huzuni zinazo onyesha ukubwa wa mapenzi yao pamoja na kushikamana kwao na mafundisho ya Imamu Swadiq (a.s), yaliyo jaa utukufu, kujitolea na ukarimu, ambayo ni muendelezo wa mafundisho ya babu yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w), na wanalichukulia tukio hili kama taa linalo waongoza katika njia huku wakiwa na majonzi makubwa.
Kumbuka kua Ataba tukufu za Karbala hufanya matembezi ya kuomboleza katika kumbukumbu za vifo vya watu wa nyumba ya Mtume (a.s) katika kipindi chote cha mwaka, na matembezi hayo huanzia katika Atabatu Husseiniyya kwenda Atabatu Abbasiyya au kinyume chake.