Kitengo cha mitambo (usafirishaji) cha Atabatu Abbasiyya tukufu chaandaa gari (15) kwa ajili ya kubeba zaidi ya wanafunzi (500) wanao kwenda kufanya mitihani…

Maoni katika picha
Miongoni mwa kazi za kibinadamu zinazo fanywa, ni hii ya kupunguza tabu ya usafiri kwa wanafunzi wa kike wanao fanya mitihani katika vituo vya mbali na maeneo wanayo ishi, ili kuwafanya wavuke hatua hii salama, kitengo cha mitambo (usafirishaji) cha Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya maelekezo ya uongozi wake mkuu, imechukua jukumu la kuwapa usafiri wanafunzi wanaoishi mbali na vituo vya mitihani, wanapelekwa katika vituo vya mitihani na kurudishwa majumbani kwao.

Jambo hili kwa mujibu wa maelezo ya makamo rais wa kitengo cha usafirishaji Ustadh Maitham Abdul-Amiir: “Sio la mara ya kwanza, Kitengo cha usafirishaji cha Atabatu Abbasiyya kimekua kikifanya jambo hili, hususan kusaidia usafiri wa wanafunzi wanao ishi katika maeneo yaliyopo mbali na vituo vya kufanyia mitihani, na inakua tabu kwao kufika katika vituo hivyo ambavyo vipo kwenye majengo ya Maahadi ya ufundi katika mkoa wa Karbala, wameandaa gari (15) kubwa zenye uwezo wa kubeba watu (50) na ndogo zenye uwezo wa beba watu (25)”.

Akaongeza kua: “Jambo hili la kutoa usafiri kwa wanafunzi limefanyika baada ya makubaliano na viongozi wa shule wanazo toka bamoja na wazazi wao, na vimeainishwa vituo ambavyo ni rahisi kwa kukusanyika na kupitiwa na gari zetu ambazo zinawapeleka na kuwarudisha, kazi hii imeanza tangu siku ya mtihani wa kwanza na itaendelea hadi mtihani wa mwisho”.

Wanafunzi pamoja na wazazi wao wametoa shukrani kubwa kwa Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kuwapa msaada huu ambao uwewawezesha kufika mapema katika vituo vya mitihani, na kurudi mapema majumbani kwao bila kupata usumbufu wa usafiri wala mateso ya jote.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: