Miongoni mwa orohda za nadwa zake katika kumbukumbu ya kifo cha Imamu Swadiq (a.s), Maahadi ya Qur’an tukufu ya Atabatu Abbasiyya ilifanya nadwa ya Qur’an katika wilaya ya Hindiyya iliyo hutubiwa na Sayyid Rashidi Husseini ambaye alizungumza mada ya: “Imamu Swadiq (a.s) na kupinga kutafsiri kwa rai”, na kuhudhuriwa na idadi kubwa ya wasomi wa dini na wa kisekula.
Nadwa ilijikita katika kuangalia nafasi ya Imamu Swadiq (a.s) katika kupambana na fikra mbalimbali na kuifanyia kazi Qur’an tukufu, na namna alivyo kua na utaratibu maalumu wa kuamiliana na jambo hili, ni lazima tufuate utaratibu huo katika kujenga umma na kujitenga na milengo au ijtihadi za rai na kuisemea Qur’an mambo yasiyo stahiki, jambo hilo ni tofauti na mwenendo wa Ahlulbait (a.s), akasisitiza kua umma unahitaji kuwa na vijana wenye kujitambua na kuwafundisha Qur’an kama hatua ya kwanza kisha waifanyie kazi, hatuwezi kuifanyia kazi Qur’an kama bado hatujaifahamu, ni muhimu (kuifundisha Qur’an na kuifanyia kazi) ndio lendo la mradi mkubwa unao waelekeza watu katika mwenendo wa vizito viwili.
Kiongozi wa tawi la Maahadi katika wilaya ya Hindiyya Sayyid Haamid Mar’abi ametuambia kua: “Kufuatia kumbukumbu ya kifo cha Imamu Swadiq (a.s), tawi la Maahadi limeamua kufanya nadwa hii, ambayo ni moja ya nadwa za kila mwezi na hualikwa wasomi mbalimbali wa Qur’an na viongozi wa hauza na wa sekula, kwa lengo la kueneza elimu ya kitabu kitukufu na kufanyia kazi mafundisho yake kwa mujibu wa mtazamo sahihi”.
Kumbuka kua Maahadi ya Qur’an tukufu hufanya nadwa mbalimbali na semina za Qur’an pamoja na miradi mbalimbali inayo husu Qur’an kwa ajili ya kueneza uwelewa wa Qur’an katika jamii.