Idara ya shule za wasichana za Alkafeel yahitimisha semina ya bibi Amina bint Wahabi (a.s) na yatangaza semina nyingine siku za mbele…

Sehemu ya semina
Idara ya shule za wasichana za Alkafeel ambazo zipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu iliyopo katika kituo cha Swidiqah Twahirah (a.s) imefanya hafla ya kufunga semina ya Amina bint Wahabi (a.s), ambayo ni semina ya kidini iliyopo katika orodha ya semina zinazo fanywa na idara hiyo, semina hii ilikua na washiriki (280) wenye umri kati ya miaka (8-17), mambo yaliyo fundishwa katika semina hii yamepangiliwa vizuri na jopo la wabobezi wa uelimishaji rika, na zimewasilishwa na watalamu wenye uzowefu mkubwa wa kuongea na akili za umri huo.

Hafla ya kufunga semina imefanyika katika ukumbi mkuu wa kituo cha Swidiqah Twahirah (a.s), kiongozi wa kituo Ustadhat Ummu Sajjaad alitoa ujumbe, ambapo aliwashukuru wanafunzi kutokana na juhudi zao za kufatilia masomo, na akawahimiza kuongeza juhudi katika kutafuta elimu na kuyafanyia kazi mambo waliyo soma katika semina hii yenye umuhimu kwenye maisha yao ya nyumbani na shuleni, pia aliwapongeza wasimamizi wa semina kwa kazi nzuri walizo fanya kipindi chote cha semina, akabainisha kua kituo kitaendelea kuandaa na kusimamia semina zingine siku zijazo.

Hafla ilipambwa na kaswida na mashairi kutoka kwa washiriki na ikahitimishwa kwa kugawa vyeti vya ushiriki kwa wanasemina, huku shukrani nyingi zikielekezwa kwa Atabatu Abbasiyya na viongozi wa idara ya shule za Alkafeel.

Kumbuka kua hii ni miongoni mwa semina zinazo endeshwa na Atabatu Abbasiyya tukufu inayo lenga kufundisha maadili mema kwa vijana, katika semina hii yamefundishwa masomo mbalimbali kama vile (Fiqhi, Aqida, Akhlaq, Sira, Mambo ya kifamilia, kazi za mikono, Uchoraji na michezo), vilevile imetolewa mihadhara tofauti, pamoja na kuswali swala za jamaa kila siku na kuonyesha filamu inayo elezea historia ya mmoja wa Maimamu (a.s) au swahaba mtukufu, sambamba na kuwepo kwa safari za mapumziko katika baadhi ya maeneo ya Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: