Kikosi kinacho rusha matangazo ya moja kwa moja (mubashara) chini ya kituo cha Alkafeel cha Atabatu Abbasiyya tukufu, wamefanya juhudi kubwa ya kurekodi majaalisi za maombolezo zilizo fanywa na kikosi wa Abbasi (a.s) cha wapiganaji, zilizo endelea kwa zaidi ya siku sita katika mikoa mitatu tofauti, ambayo ni: Diyala, Karkuuk na Basra, waliandaa mahitaji yote ya kiufundi na wakachukua picha nzuri sana zilizo rushwa na vituo mbalimbali vya luninga (tv) kupitia masafa ya Atabatu Abbasiyya tukufu ya bure.
Kiongozi wa kituo Ustadh Bashiri Taajir ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Hakika watalamu wa kituo cha Alkafeel wana uzowefu mkubwa unao wawezesha kufanya kazi yeyote kwa ustadi na ubora mkubwa, wametoa picha zilizo rushwa na chanel mabalimbali za luninga (tv), wameweza kuturushia majaalisi za kumbukumbu ya kifo cha Imamu Swadiq (a.s), na kuonyesha hali halisi ya majlisi hizo zilizo simamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, zilizo kua na mihadhara iliyo kua inatolewa na Shekh Zamaan Hassanawi, pamoja na matam zilizokua zinasomwa baada ya muhadhara”.
Akaongeza kua: “Majaalisi za kuomboleza zilipata mwitikio mkubwa kutoka kwa wapenzi na wafuasi wa Imamu Swadiq (a.s), hususan katika miji ambayo majaalisi hizo zimefanywa kwa mara ya kwanza baada ya kuwatimua magaidi ya Daesh na kukombolewa miji hiyo, jambo hilo lilipelekea kua na mwitikio mkubwa sana hususan katika mji wa Bashiir”.
Akaongeza kusema kua: “Matukio yalianza kurushwa siku mbili kabla ya siku aliyo fariki na siku moja baada ya siku aliyo fariki, katika mkoa wa Basra ambao majaalisi zilisimamiwa na kikundi cha Mwezi wa bani Hashim (Qamaru Bani Haashim) na zilikua zikihutubiwa na Shekh Haidari Maula”.