Dondoo za kumbukumbu ya kuzaliwa kwa bibi Fatuma Maasuma (a.s)…

Maoni katika picha
Pamoja na kuwa mwezi wa Dhulqa’ada una utukufu mkubwa, pia unamatukio mengi, siku ya kwanza ya mwezi huo; ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa bibi Fatuma bint Imamu Mussa Alkadhim mtoto wa Imamu Jafari Swadiq (a.s) anaye julikana kwa jina la Maasuma, mjukuu wa Mtume na tawi lenye manufaa miongoni mwa matiwi ya mti mtukufu wa Alawiyya, mjukuu wa Swidiqah Zaharaa (a.s) mwingi wa kufanya ibada.

Bibi Maasuma alizaliwa siku ya kwanza ya mwezi wa Dhulqa’ada mwaka wa 173h katika mji wa Madina, imepokewa kua kaka yake Imamu Ridha (a.s) ndiye aliyempa jina la “Maasuma” pia imepokewa kuwa babu yake Imamu Swadiq (a.s) alimpa jina la “Karimatu Ahlulbait” kabla ya kuzaliwa na mama yake aitwaye Tuktam aliye kua kijakazi.

Bibi Maasuma alilelewa na kaka yake Imamu Ridha (a.s), kwa sababu Haruna Abbasiy alimuweka jela baba yake katika mwaka wa kuzaliwa kwake, na akamuua kwa sumu mwaka wa 183h, akaishi pamoja na ndugu zake chini ya uangalizi wa Imamu Ridha (a.s), hadi Maamun alipo mtaka aende katika mji wa Khurasan, wakabaki na hofu kubwa kuhusu usalama wake, hususan pale alipo waambia kua atafariki katika safari hiyo ya kwenda Tusu, bibi Maasuma hakuweza kuvumilia kuishi mbali na kaka yake, akafunga safari ya kumfuata, akiwa na matumaini ya kukutana naye akiwa hai, lakini safari ilikua ndefu na ilimchosha, akaugua akiwa safarini ikabidi alale huku anaugulia.

Akabebwa hadi katika mji wa Qum akiwa mgonjwa, akafia katika mji huo baada ya siku kumi na saba, ilikua tarehe kumi ya mwezi wa Rabiu-Thani mwaka 201h, na akazikwa katika mji wa Qum na kaburi lake lipo hadi leo, kaburi lake lilijengewa banda, hadi alipo kuja bibi Zainabu bint Imamu Muhammad Jawaad (a.s) akamjengea kubba, na zikaonekana karama nyingi katika kaburi la bibi Maasuma, baadhi ya karama hizo zimenukuliwa na muandishi wa kitabu cha (Karaamaati Maasumiyya), kwenda kumzuru kuna utukufu mkubwa na thawabu nyingi, kuna riwaya nyingi zinazo elezea utukufu wa kumzuru bibi Fatuma (a.s) miongoni mwa riwaya hizo ni:

  • 1- Kutoka kwa Sa’adi bun Saidi, kutoka kwa Abu Hassan Ridha (a.s) anasema: Nilimuuliza kuhusu kaburi la Fatuma bint Mussa bun Jafari (a.s) akasema: (Atakaye mzuru (mtembelea) ataingia peponi).
  • 2- Imamu Jawaad (a.s) anasema: (Atakaye zuru kaburi la shangazi yangu katika mji wa Qum ataingia peponi).
  • 3- Kutoka kwa Sa’adi, kutoka kwa Imamu Ridha (a.s) anasema: (Ewe Sa’adi, kuna kaburi letu kwenu, nikasema: Kaburi la Fatuma bint Mussa? Akasema: Ndio, Atakaye litembelea huku anajua utukufu wake ataingia peponi).
  • 4- Imamu Swadiq (a.s) anasema: (Hakika Mwenyezi Mungu ana haram nayo ni Maka, na Mtume (s.a.w.w) anaharam nayo ni Madina, na Amirulmu-uminina (a.s) ana haram ambayo ni Kufa, na sisi tuna haram nayo ni Qum, atazikwa katika mji huo mwanamke katika kizazi changu aitwae Fatuma, atakaye mtembelea ataingia peponi).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: