Kwa picha: Kukamilika kwa kazi ya uwekaji wa marumaru katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na milango yake imefunguliwa kuwapolea mazuwaru…

Maoni katika picha
Kazi ya kuweka marumaru katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) imekamilika ndani ya muda ulio pangwa, zimewekwa marumaru adimu sana kwa ajili ya kukanyagwa na watu watukufu wanaokuja kumzuru Abulfadhil Abbasi (a.s), katika eneo linalo kadiriwa kuwa na ukubwa wa mita za mraba 1000, zilizo gawanywa kwa ukubwa sawa baina ya upande wa wanawake na upande wa wanaume.

Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi cha Atabatu Abbasiyya ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Uwekaji wa marumaru katika haram ya Abulfadhil Abbasi ni sehemu muhimu katika mradi wa uwekaji wa marumaru ndani ya uwanja wa haram tukufu ambao umegawanywa katika hatua kadhaa, hatua ya kwanza ilihusisha kuweka marumaru sehemu maalumu ya upande wa wanawake, baada ya kumaliza tukaja kuweka upande wa wanaume, kwa kumaliza sehemu hizo mbili, hatua ya uwekaji marumaru inakua imekamilika. Na milango imefunguliwa kwa ajili ya kuwapokea mazuwaru, sasa tutaelekea katika uwanja wa haram tukufu chini ya utaratibu ulio pangwa, ambapo marumaru zitawekwa kwa vipande vipande ili tusisababishe usumbufu kwa watu wanaokuja kufanya ziara”.

Akaongeza kua: “Imefanyika juhudi kubwa kwa ajili ya kukamilisha hatua hii, kitengo cha uangalizi wa kihandisi kilikua na nafasi kubwa katika hatua zote za utekelezaji wa mradi huu, kuanzia kutoa marumaru za zamani hadi uwekaji wa marumaru hizi mpya”.

Akabainisha kua: “Marumaru mpya zilizo wekwa zina ukubwa wa (sm 40x40) na unene wa (sm 3) za aina ya (Multi Onyx), zilifanyiwa uchunguzi wa kina wa kihandisi kuhusu uimara wake na umadhubuti wa rangi yake pia zina sifa zingine za ziada zinazo zifanya marumaru hizo kua bora zaidi”.

Akafafanua kua: “Marumaru zenye rangi zimepangwa vizuri kutokana na muelekeo wa dirisha la Abulfadhil Abbasi (a.s), pamoja na ukuta wa haram yake, kazi hii ilitanguliwa na kufanyiwa usafi haram tukufu pamoja na kukarabati sehemu zote ikiwemo kuandaa ardhi kwa kuweka baadhi ya vitu vinavyo rahisisha na kuimarisha ukaaji wa marumaru juu yake”.

Fahamu kua kazi zilizo fanywa kabla ya kuweka marumaru mpya ni:

  • - Kutoa marumaru za zamani.
  • - Kuondoa baadhi za sehemu ya zege ya zamani na kurekebisha sehemu zilizo haribika.
  • - Kumwaga zege katika ardhi (sakafu) yenye viwango maalumu vinavyo iwezesha kushikana vizuri na zege ya zamani na kuzuiya unyevunyevu.
  • - Limetengenezwa tabaka la chuma chini ya zege.
  • - Umetengenezwa mtandao wa kusambaza maji, wa mawasiliano, wa kuzuia moto na wakutoa tahadhari, na kuiunganisha na mitandao mikuu ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Kumbuka kua haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) imeshuhudia utekelezwaji wa miradi mingi, katika vipindi tofauti, kila uradi ulikua na umuhimu sawa na mwingine, mtiririko wa miradi hiyo unakamilishwa na mradi wa kuweka marumaru katika haram tukufu ambayo kwa mara ya mwisho iliwekwa marumaru katika miaka ya sabini karne iliyo pita.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: