Atabatu Abbasiyya tukufu yafanya semina yenye washiriki 45 kutoka katika vyuo vikuu 16 kuhusu mtazamo wa nguvu ya ubongo…

Maoni katika picha
Miongoni mwa mfululizo wa semina za kitalamu zinazo lenga kubadilishana uzowefu na vyuo vikuu vya kimataifa, Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa semina kuhusu (Mtazamo wa nguvu ya ubongo), kwa ajili ya kujenga mawasiliano ya kielimu kati ya Ataba tukufu na taasisi za elimu, pamoja na kufungua uwanja mpya utakao saidia kupata haraka maendeleo mapya ya kielimu katika fani zote.

Semina imefanyika ndani ya ukumbi uliopo katika jengo la Haadi (a.s) ikiwa na washiriki 45 kutoka vyuo vikuu 16, wakiwa ni wakufunzi wa vitivo (michepuo) torauti, ni semina ya siku nane, chini ya ukufunzi wa Dokta Shaamil Haadi Muhsin ambaye ni mwakilishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu nchini Marekani na mkufunzi wa chuo kikuu cha Okland cha Marekani.

Masomo yatakayo fundishwa ni pamoja na kuangalia chembechembe za ubongo, na namna ya kufanya upasuaji katika ubongo, ambao ni utafiti unaofanywa na jopo la wasomi wa kimarekani, akiwemo mkufunzi wa semina hii, pia wataonyesha namna ya kutengeneza kizazi cha wenye akili, na ataonyesha namna ya kupandikiza chembechembe hai katika damu na kwenye ubongo, na namna zinavyo fanya kazi ya kutuma ishara pamoja na mabadiliko ya kinafsi yanayo tokana na ishara hizo, na njia za elimu mpya katika utafiti wa nguvu za ubongo na namna unavyo fanya kazi ya kukusanya taarifa na kuzipangilia chini ya utaratibu maalumu tena kwa umakini wa hali ya juu kabisa na kutoa jibu stahiki ndani ya muda mfupi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: