Kitengo cha uangalizi wa kihandisi chakamilisha matengenezo ya moja ya majengo ya vyoo…

Maoni katika picha
Kitengo cha uangalizi wa kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu kinaendelea na kazi ya matengenezo katika majengo yote ya vyoo, vya ndani na nje, kwa ajili ya kuhakikisha wanatoa huduma bora zaidi kwa mazuwaru, hivi karibuni wamekamilisha matengenezo ya moja ya jengo la vyoo linalo tumiwa na idadi kubwa ya mazuwaru, hususan karika siku za ziara za milionea (zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu), hiyo ni sababu ya kudumisha matengenezo katika vyoo hivyo kutokana na kutumika kwake wakati wote.

Rais wa kitengo cha uangalizi wa kihandisi Muhandisi Abbasi Mussa ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Matengenezo ya jengo hili ni miongoni mwa orodha ya kazi za kitengo hiki, jengo lina ghorofa tatu, eneo lake linaukubwa wa mita za mraba (360), lina idadi kubwa ya vyoo vya wanaume na wanawake, matengenezo yamehusisha utengenezaji wa ukuta na sakafu pamoja na kuweka marumaru mpya”.

Akaongeza kua: “Vile vile matengenezo haya yamehusisha, mfumo wa umeme, maji (bomba za maji) pamoja na mfumo wa maji taka, limefanyiwa matengenezo paa na kufunga taa za kisasa pamoja na kuweka milango mipya, na kukarabati sehemu za kuchukulia udhu, hivi sasa vyoo vinamuonekano mpya na vipo tayali kutumiwa na mazuwaru”.

Tunapenda kukumbusha kua kitengo cha uangalizi wa kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu, ni miongoni mwa vitengo muhimu sana, kina idara nyingi na ofisi mbalimbali, kina mafundi na wahandisi wanao fanya kazi usiku na mchana katika vitengo vyote vya Atabatu tukufu kwa ajili ya kuhakikisha wanatoa huduma bora zaidi kwa mazuwaru watukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: