Kwa ushiriki wa watu (75): Mashindano ya Karbala ya waimbaji wa Husseiniyyiin yakamilika…

Maoni katika picha
Jioni ya Juma Tano (18/07/2018m) sawa na (3 Dhulqa’ada 1439h) yalihitimishwa mashindano ya Karbala ya waimbaji wa mimbari za Husseiniyya, yaliyo simamiwa na kamati ya washairi na waimbaji wa mji wa Karbala chini ya ufadhili wa Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya pamoja na kitengo cha habari na utamaduni cha Ataba tukufu.

Hafla ya kufunga mashindano hayo yaliyo dumi siku nne na kua na washindani (75) wote wakitoka katika mkoa wa Karbala, ilifanyika ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s), ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu iliyo somwa na msomaji wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Badri Mamitha, kisha ukafuata ujumbe wa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya ulio wasilishwa na Shekh Ali Muhaan, ambaye alisema kua: “Nakufikishieni salamu za kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, nakufikishieni pia dua yake kwenu anayo kuombeeni muwe na mafanikio ya kudumu”, akaongeza kua: “Hakika kumtumikia Imamu Hussein (a.s) na kufanya kila jambo linalo husiana nae, ni sawa na kumtumikia Mwenyezi Mungu mtukufu, kupitia kazi hizi tunatarajia kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu mtukufu”.

Akabainisha kua: “Mmepata taufiq ya Mwenyezi Mungu mtukufu, kwa kumtumikia Imamu Hussein (a.s) kwa njia hii, wengine wanajitahidi pia kumtumikia Imamu Hussein (a.s) lakini kwa kupitia njia zingine, na wote mnategemea taufiq ya Mwenyezi Mungu, mmepata utukufu mkubwa sana kwa kufanya kazi hii, na jambo muhimu kwenu ni kubakia katika njia hii, namuomba Mwenyezi Mungu mtukufu muendeleze njia hii na kuitunza isipotee, msije mkaifananisha kazi hii na kazi nyingine yeyote hapa duniani, hii taufiq kubwa sana mliyo pata shikamaneni nayo kwa nguvu zote”.

Kisha ukafuata ujumbe wa kitengo cha habari na utamaduni ulio wasilishwa na makamo rais wa kitengo hicho Sayyid Aqiil Yasiri, naye alisema kua: “Kuna hadithi kutoka kwa Imamu Swadiq (a.s) inasema: (Huisheni mambo yetu Mwenyezi Mungu amrehemu atakaye huisha mambo yetu), kuhuisha jambo wakati mwingine inakua kwa vitendo, na atakaye pata bahati ya kumtumikia Imamu Hussein (a.s) na Maulana Abulfadhil Abbasi pamoja na Maimamu wengine watakatifu (a.s), hakika ni wajibu wetu kuhuisha mambo yao, na nyie mmepata nafasi hiyo, mnaheshima kubwa katika kutoa huduma ya kuhuisha mambo yao kwa kufanya majaalisi (vikao) na kusoma matam na nauha (mashairi na kaswida) kuhusu Maimamu watakasifu, kuanzia Mtume (s.a.w.w) hadi Imamu Mahdi Almuntadhar (a.f).

Akaongeza kusema kua: “Hakuna mshindi na aliye shindwa katika mashindano haya, pamoja na kua hiyo ndio kawaida ya mashindano, kuna atakaye watangulia wenzake na kuna watakao kua nyuma lakini huu sio mwisho, wote mmesha sajiliwa kwa Imamu Hussein (a.s) watumishi, waimbaji na waombolezaji wa watu wa nyumba ya Mtume (a.s), wote mnatakiwa mpate furaha, kamati ya majaji imeangalia vipengele vyote vya mashindano kwa mazingatio makubwa”.

Akaongeza kua: “Mimi ninaelimu ndogo kuliko nyie na ninadhambi nyingi zaidi yenu, sitaki kukupeni nasaha bali nauhusia nafsi yangu, mwanadamu anatakiwa ajitahidi kadri ya uwezo wake, hususan anapokua mwimbaji (wa mimbari Husseiniyya) kwa sababu akipanda katika mimbari watu wote wanamtazama yeye, anatakiwa apambike kwa tabia za watu wa nyumba ya Mtume (a.s), pia anatakiwa aangalie mavazi yake, ukataji wa nywele na anapo ongea basi aongee maneno yanayo mridhisha Mwenyezi Mungu mtukufu, asiyazingatie hayo katika majlisi pekeyake bali kila sehemu, inatakiwa mwenendo wetu na vitendo vyetu tuishi kana kwamba tupo katika mimbari wakati wote, mwimbaji wa mimbari Husseiniyya lazima awe na tabia nzuri wakati wote na kila mahala, tusidanganywe na mazingira. Nyie wote mmefanya vizuri, katika siku hizi nne za mashindano tumemuangalia mshiriki mmoja mmoja, kila mmoja miongoni mwenu anasifa za pekee tofauti na mwingine, tunakuombeeni mdumu katika wema na Mwenyezi Mungu akupeni kila la kheri”.

Halafu ukafuata ujumbe kutoka katika kamati ya majaji, ulio wasilishwa na mjumbe wa kamati hiyo mwimbaji Abdul-Amiir Al-Umawiy Al-Karbalai, ambaye alisema kua: “Leo tumekutana kutoa kizazi kipya cha watumishi wa Hussein (a.s) ambao ni mwendelezo wa kizazi cha zamani kilicho kua kikiendesha mimbari za Husseini (a.s), asilimia kubwa ya waimbaji wa mbimbari za husseini hawajasomea chuo chochote, bali wameiga katika mimbari za Hussein hapa Karbala, hakika mtumishi wa Imamu Hussein (a.s) anajukumu kubwa, anaangaliwa kila kitendo anacho fanya au kauli anazoongea, kamati hii mnayo iona imesha toa wahitimu wengi”.

Akaongeza kua: “Nawashukufu sana ndugu zetu watukufu walio toa mafunzo katika mitaa na maeneo ya mji wa Karbala, miongoni mwao kuna ambao wapo tayali na tunanufaika na matunda yao, nao ni wale wanao imba katika majlisi za Husseiniyya hapa Karbala, tunawashukuru sana ndugu zetu walio shiriki katika mashindano haya, katika hili washindane wenye kushindana”.

Baada ya hapo vikaibwa vipande vya kaswida murua na mshindi wa mashindano haya, Mwimbaji Ali Waailiy, kisha kamati ya majaji ikapewa zawadi, ambayo inaundwa na:

  • 1- Mshairi mtaalamu Auda Dhwahi Karbalai.
  • 2- Mshairi na mwimbaji Abdul-Amiir Al-Umawiy Al-Karbalai.
  • 3- Mshairi Abdul-Rasuul Khafaaji.
  • 4- Mshairi mtaalamu Mahdi Hilali Karbalai.
  • 5- Mshairi Farasi Asadi Karbalai.

Halafu washindi wa mashindano wakapewa zawadi sambamba na kugawa vyeti kwa washiriki wote wa mashindano. Kitengo cha habari na utamaduni nacho kikagawa midani kwa watu waliokua na mchango mkubwa wa kufanikisha mashindano haya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: