Idara ya wahadhiri wa kike katika Atabatu Abbasiyya tukufu yatangaza kufanyika kwa mashindano ya kitafiti na yatowa wito kwa watafiti wa kike waje kushiriki…

Maoni katika picha
Idara ya wahadhiri wa kike katika Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza azma yake ya kufanya nadwa ya kitafiti na mashindano rasmi mwezi ishirini Dhulhijja chini ya kauli mbiu isemayo: (Khutuza za wanawake baina ya uhalisia na utendaji) na anuani ya mashindano hayo inasema: (Kutoka kwa Imamu Hussein –a.s- tunapata ujasiri na kujitolea… na kutoka kwa Marjaiyya tunapata msimamo na ushindi), imetoa wito kwa watafiti wa kike wajitokeze kushiriki kwa kuandaa tafiti zinazo endana na mada zilizo pangwa, ambazo ni:

Mada ya kwanza: Khutuba za wanawake na athari yake katika kuimarisha itikadi ya kiislamu, bibi Zaharaa (a.s) kama mfano.

Mada ya pili: Jukumu la khatibu (mzungumzaji) wa kike katika kumuandaa mama mwema na mlezi bora, bibi Zainabu (a.s) kama mfano.

Mada ya tatu: Nafasi ya mhadhiri wa kike katika kubainisha fatwa ya ushindi na msimamo, bibi Ummul Banina (a.s) kama mfano.

Mada ya nne: Khutuka (mawaidha) ya wahadhiri wa kike na athari zake katika kulinda mshikamano wa familia, bibi Fatuma Maasuma (a.s) kama mfano.

Idara imebainisha masharti ya kushiriki katika nadwa hii ambayo washindi watapewa zawadi baada ya kuchujwa tafiti zao na kamati ya majaji, masharti ni kama yafuatayo:

  • - Utafiti usiwe umesha wahi kutolewa na watu wengine kabla yake.
  • - Utafiti uandikwe kwa kufuata kanuni za kielimu.
  • - Usiwe chini ya kurasa 15 na sio zaidi ya kurasa 30.
  • - Saizi ya maandishi iwe 16 na uwekwe kwenye (CD) pamoja na wasifu (cv) ya muandishi, na ahakikishe utafiti wake hauzidi maneno 300.
  • - Utafiti wowote ambao hautaendana na mada tulizo taja hautapokelewa, au ambao hauta ambatanishwa na wasifu wa muandishi.
  • - Tafiti zipelekwe moja kwa moja katika ofisi ya wahadhiri wa kike ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu au zitumwe kwenye namba ya simu (07810645244) kupitia Telegram.

Kumbuka kua lengo la kufanya nadwa hii ya mashindano ni kuongeza uwezo wa wahadhiri wa kike katika jamii yetu, na kuwafahamisha majukumu yao katika mwezi wa Muharam na Safar, pamoja na kuandaa mazingira mazuri ya kufundisha uislamu sahihi wa Mtume wa Mwenyezi Mungu na Amirulmu-uminina (a.s), na umuhimu wa kufanya maadhimisho ya Husseiniyya na kuyaenzi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: